NIDA WATOA NJIA RAHISI YA KUPATA NAMBA YA KITAMBULISHO MTANDAONI



Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imewarahisishia  wananchi kwa kuweka utaratibu mpya wa kuipata namba ya utambulisho wa Taifa (NIN)  kwa njia ya mtandao.

Taarifa iliyotolewa na Nida jana Jumatano Septemba 25, 2019 kupitia kitengo cha mawasiliano na hifadhi hati ilisema namba hiyo sasa imeanza kutolewa kupitia tovuti ya mamlaka hiyo kwa muombaji kutembelea>>> https://services.nida.go.tz/nidpotal/get_nin.aspx

Taarifa ya Nida ilibainisha kwamba huduma hiyo itawarahisishia waombaji wa vitambulisho vya Taifa kupata NIN bila kwenda ofisi za mamlaka hiyo.

Hatua za kufuta kupata namba ya NIN

1.Bonyeza kitambulisho cha Taifa

2.Fahamu namba ya utambulisho wa Taifa

3.Andika jina lako la kwanza, jina la ukoo, tarehe ya kuzaliwa, jina la kwanza la mama na jina la mwisho la mama

4.Bonyeza Tafuta

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?