WhatsApp yafuata nyayo za Facebook matangazo ya kibiashara
WhatsApp yaja kivingine yaanza kutumia matangazo kujiingizia kipato. Picha|Mtandao. Mtandao huo umetangaza kuwa utaanza kuweka matangazo ya kibiashara katika kurasa zake ifikapo 2020. Matangazo hayo yataanza kuonekana kwenye “Status stories”. Dar es Salaam. Hatimaye Mtandao wa WhatsApp umechukua hatua mpya ya kujiingizia kipato, baada ya kutangaza kuanza kupokea matangazo ya kibiashara kuanzia mwaka 2020. Mtandao huo umbao uko chini ya umiliki wa Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg utaanza kuweka matangazo hayo kwenye ‘status stories’ ili kuwafikia watu wengi kirahisi. Taarifa ya WhatsApp kujitosha katika matangazo ya kibiashara kama ilivyo kwa Facebook na Instagram imetolewa katika Mkutano wa mwaka wa Masoko wa Facebook nchini Uholanzi . Katika kufanikisha hilo mtandao huo wenye watumiaji wapatao bilioni 1.5 ulimwenguni utaongeza kitu kipya ifikapo mwaka 2020 ambapo kupitia matangazo ya ndani ya WhatsApp ( WhatsApp's 'Status-stories') wataanz...