Posts

Showing posts from October, 2018

Wema atikisa wizara ya Sana'a, naibu waziri ateta

Image
Friday, October 26, 2018 Alichokisema Naibu Waziri wa Habari Juliana Shonza Kuhusu Sakata la Wema Sepetu Kusambaza Video Chafu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza *** Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo ameitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu kusambaa kwa picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii. Akiongea na kituo cha runinga cha EATV, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza amesema wameanza kuwachukulia hatua wasanii wote waliochapisha video zenye maudhuhi ya picha za ngono mitandaoni. Kwa upande mwingine, Mhe. Shonza amesema kuwa licha ya wasanii hao kuhojiwa na Bodi ya  filamu pia watahojiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

PICHAZ: HALI ILIVYO NYUMBANI KWA MO DEWJI

Image
HII ni taswira halisi ya nyumbani kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji (MO) maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam ambaye ametekwa leo alfajiri katika eneo ambalo anafanyia mazoezi kila siku (GYM) Colosseum iliyopo maeneo ya Masaki. Tumeweza kufika eneo amablo anaishi na kuangalia hali halisi ya kwake na kukuta ulinzi mkali unaendelea nyumbani kwake hapo. Picha kwa hisani ya Global

Wanafunzi kupewa usafiri wao binafsi Dar

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema serikali ya Mkoa huo ipo katika mikakati ya kuingiza magari 20 maaulum kwa ajili ya wanafunzi wa mkoa huo ili kuwaondolea adha ya usafiri na kuwapa fursa ya kuwahi masomoni hususani nyakati za asubuhi. Makonda ameyasema hayo leo alipotembelea kituo cha mabasi yaendayo haraka kilichopo Kimara, Dar es salaam, ambapo ameahidi kulitatua suala la usafiri lililojitokeza kituoni hapo sambamba na kumaliza tatizo la usafiri kwa upande wa wanafunzi wa mkoa wa Dar es salaam kwa kuwapatia magari yao binafsi. “Kuna changamoto ya wanafunzi wanapata shida ya usafiri na wengi wao ni watoto, sisi kama serikali ya Mkoa tuna mpango wa kuingiza magari 20 maalumu kwaajili ya wanafunzi wetu ili watoto hao waweze kupata fursa ya kuwahi masomoni, na mpango huo endapo wakubwa zetu wakikubali tutaanza kutumia barabara za mwendokasi”, amesema Makonda. Aidha Makonda amewaomba wananchi wanaotumia usafiri wa mwendokasi kuipatia serikali muda...

Updates za Mchana: Polisi Yasema Mo Dewji Bado Hajapatikana, Oparesheni Kali ya Kumtafuta Bado Inaendelea

Image
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amezungumza mchana huu kuhusiana na tukio la kutekwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mo Dewji ambapo amesema hadi mchana huu taarifa rasmi ni kwamba Mo bado hajapatikana na watekaji bado hawajakamatwa. Mambosasa amewataka wananchi kuzipuuza taarifa zinazosambaa mitaani kwamba Mo kapatika akiwa Coco beach kwa kuwa ni za uongo na wala hazijatolewa na ofisi yake. Amesema jeshi la polisi linaendelea na Opareshen kali kwa kushirikisha mikoa mitatu kuhakikisha Mo Dewji anapatikana na watekaji wanatiwa Mbaroni