Waitara Asema Kilichomuondoa CHADEMA ni Ugomvi Kati yake Na Mbowe Baada ya Kumtaka Asigombee Tena Uenyekiti wa Chama Hicho

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara amesema kilichosababisha kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM ni Uenyekiti. Waitara ametangaza uamuzi wa kujiunga na CCM leo Julai 28 katika mkutano na wanahabari uliofanyika Ofisi za CCM, Lumumba. “Shida ni uenyekiti wa Chadema, ukianzia kwa akina Chacha Wangwe, Zitto Kabwe, hata mimi ni uenyekiti hapo kuna shida,” amesema. Amesema suala la uenyekiti sio lake peke yake bali wapo wabunge wengi wanaoguswa nalo lakini hataki kuwataja kwa majina. “Kuna kikao tulikaa na wabunge wengi wa majimbo na viti maalumu tukawa tunazungumza kwamba Tundu Lissu agombee uenyekiti baadaye hoja hiyo wakaicha mimi nikaendelea nayo. Wakaniambia ninataka Tundu Lissu agombee au ni mimi mwenyewe?” amesema na kuongeza: “Mbowe amewahi kuniambia kamanda unanipinga na mimi ntakushughulikia na kwenye Chadema bado hakuna mtu kama yupo ntamng'oa hikii chama ni mali yangu.” Waitara amesema kwamba ugomvi huo uliibuka kwa sababu mchakato wa Uch...