WAUAJI WA BILIONEA MSUYA WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha, imewahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa watano baada ya kukutwa na hatia ya kumuua kwa makusudi aliyekuwa mfanyabiashara wa Arusha na Mirerani mkoani Manyara, Erasto Msuya.
Erasto Msuya enzi za uhai wake..
Waliohukumiwa adhabu hiyo ni mshitakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed; mshitakiwa wa tatu, Mussa Mangu; wa tano, Karim Kuhundwa; wa sita Sadick Mohamed na wa saba; Ally Mussa Majeshi.
Hukumu hiyo imetolewa leo Julai 23, 2018 na Jaji Salma Maghimbi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo. Aidha, Mahakama imemwachia huru mshitakiwa wa pili, Shwaibu Jumanne baada ya kukosekana ushahidi dhidi yake.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?