BABA, NIMEPOKEA TAARIFA ZA KUPOTEA KWA NONDO






Baba Mzazi wa Abdul Nondo (Aliyepo Pichani) asema amezipokea taarifa za mtoto wake kupotea,  aonyeshwa kusikitishwa asisitiza kuwa anungana na ndugu zake kuendelea kumtafuta mtoto wake.

Asubuhi ya leo mwanafunzi mwenzetu wa chuo kikuu cha DSM comrade Abdallah Mtonda amefika nyimbani ujiji huko Kigoma kwa baba yake kumzazi ili kujua kama ana taarifa za mtoto wake Abudl kupotea. Abdalah Mtonda anaeleza kuwa baba yake ameweka wazi kuwa ni kweli amepewa taarifa za mtoto wake kupotea.

Niliombe jeshi la polisi lifanye kazi ya kulinda raia na mali zake..... Inashangazwa sana watu kila uchwao wanapotea, wanateswa na hata kuuawa na jeshi la polisi lipo.

Ikumbukwe kuwa Abdul Nondo amepotea akiwa jijini DSM usiku wa jana.

Taarifa zinaelezwa kuwa mama yake mzazi yupo DSM muda huu analia kwa majonzi makubwa kufuatia kupotea/kutekwa kwa  mtoto wake  (anasimulia  Abdalah Mtonda).

#Pichani
Abdalah Mtonda asubuhi ya leo alivyoenda nyumbani kwa Baba wa Abdul ili kujadili hatma ya Abdul Nondo.
Anaandika
©Kumbusho Dawson.

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?