SWALI” Jadili dhana ya ukumushaji na sifa zake kwa kutumia mifano sahihi.

UKUMUSHAJI
Ni dhana ambayo hutoa maelezo zaidi au
Ya ziada kuhusu nomino, kivumishi, kitenzi, kielezi au kikundi cha maneno
KIKUMISHI
Ni neno , kirai au kishazi ambacho hutoa maelezo ya ziada kuhusu nomino, kivumishi, kitenzi, kielezi au kikundi cha maneno. Aidha, kikumushi huweza kuwa sentensi itoayo maelezo zaidi kuhusu sentensi nyingine.
Mfano.
Mtoto aliyekuja juzi ameondoka.
Katika sentensi hii kishazi tegemezi “ aliye kuja juzi” ni kikumushi ambacho kinatoa maelezo ya ziada kuhusu nomino “ mtoto:.
Mwanafunzi mrefu sana ameanguka.;
Neno “sana” ni kikumushi kinachotoa maelezo ya ziada kuhusu kivumishi “ mrefu”
Mifano zaidi
Gari lilikimbia kwa kasi sana
Maduhu anaimba vizuri mno
Ninapenda unavyosema.
Mwalimu aliye kwenda dukani jana amerudi.
Kimsing ukumushaji ni dhana pana zaidi ya uvumishi, kwani ukumushaji hutoa maelelezo zaidi kuliko uvumishaji. Pia kivumishi kipo katika kategoria ya kileksika lakini kikumushi kipo katika kategoria amilifu ya isimu miundo


MAZINGIRA YA UTOKEAJI WA UKUMUSHAJI
  1. Ukumushaji unaweza kutokea baada ya nomino
Kwa mfano:
  • Kitabu kizuri kimepotea
  • Wanafunzi wapole wamefaulu mitihani yao vizuri
  • Askari katili ameuwa
  • Kijana mtiifu amezadiwa kitabu
  1. Baada ya kiwakilsishi pia kikumishi kinaweza kutokea
Kwa mfano
  • Wale watundu wamefukuzwa shule
  • Yule msafi ameondoka chuoni
  1. Kikumishi huweza kutokea baada ya kivumishi
Kwa mfano
  • Mwanafunzi mrefu kuliko wote ameanguka
  • Mwimbaji mashuhuri sana amekodiwa Uganda
  • Mwalimu mlevi kupindukiaameachishwa kazi.
  1. Vivyo hivyo kikumishi huweza kutokea baada ya kitenzi
Kwa mfano
  • Juma anaimba vizuri
  • Mbwa mkali amejeruhiwa sana
  • Ninapenda anavyocheza
  • Mwanariadha anakimbia kwa kasi
  1. Ukumushaji vilevile huweza kutokea baada ya kielezi
Kwa mfano
  • Juma anaimba polepole mno
  • Mharifu amejitetea vizuri sana
  • Mwanafunzi amewasilisha kazi kwa ujasili mwingi
  1. Ukumushaji pia huweza kutokea baada ya kihusishi
Kwa mfano
  • Janeth anakula wali kwa mkono
  • Juma amekaa juu ya meza
  • Maria analia kwa uchungu

SIFA ZA UKUMUSHAJI
  1. Hutoa maelezo ya ziada kuhusu nomino, kivumishi, kitenzi au kikundi cha maneno
Mfano:
  1. Mvulana mwembamba amepotea
Neno “ Mwembamaba” ni kikumushi kinachotoa maelezo ya ziada kuhusu nomino “ mvulana”
  1. Kijana mnene sana anacheka.
Neno “sana” ni kikumushi kinachotoa maelezo ya ziada kuhusu “kivumishi” mnene
  1. Ninapenda unavyocheza
Neno “ unavyocheza “ ni kikumishi kinachotoa malelezo ya ziada kuhusu “ kitenzi” “Ninapenda”.
  1. Mwalimu aliyekuja jana asubuhiameondoka.
Neno “aliyekuja jana asubuhi” ni kikumushi kinachotoa maelezo ya ziada kuhusu nomino “ mwalimu”
  1. Mchungaji anahubiri vizuri sana
Neno “ sana” ni kikumushi kinachotoa maelezo ya ziada kuhusu kielezi “ vizuri”
  1. Kikumushi kinaweza kuondolewa kwenye tungo bila kupoteza maana ya msingi ya tungo hiyo.
Mfano
  1. Mtoto mzuri amerudi
  • mtoto amerudi
  1. Ninapenda unavyokula
  • Ninapenda
  1. kikumushi huweza kuundwa na neno moja au kikundi cha maneno.
Mfano
  1. mtoto anacheza vizuri sana (neno moja)
  2. Msichana aliyekaa mbele yangu ni msafi (kikundi cha maneno)

  1. Kikumushi kipo katika kategoria amilifu ya isimu miundo ( mpangilio wa maneno katika tungo).
Mfano.
  1. Msichana mrembo sana anacheka
  2. Msichana mrembo anacheka
  1. Kikumushi kinaweza kutokea mara moja au zaidi katika tungo
Mfano:
  1. Ng’ombe aliyepotea jana asubuhiamepatikana leo asubuhi
  2. Msichana anacheza vizuri sana na Baba analima vizuri sana.
  1. Ukumushaji huweza kutokea kwenye kiima au kiarifu au pande zote kwa wakati mmoja
Mfano
  • Mvulana aliyetumwa kwenda kumletea mgonjwa dawa amerudi mapema mno.
  • Kijana aliyepotea jana ameonekana
  • Juma anatembea kwa madaha sana
  1. Ukumushaji huweza kutokea katika sentensi changamano ambapo kishazi tegemezi huchukua nafasi ya kikumushi
Kwa mfano
  1. Kijana aliyekuja jana ameondoka leo asubuhi
  2. Mbuzi aliyezalia porini ameletwa nyumbani
  3. Kitabu kilichoibiwa kimerudishwa
  4. Nyimbo zilizoimbwa zinafurahisha
Kwa ujumla dhana ya ukumushaji na uvumishaji kwa jinsi tulivyojadili ni dhana ambazo zinafanana katika utendaji kazi wake lakini upekee wa ukumushaji ni kwamba kivumishi huweza kutokea katika kikundi nomino pekee.
Hivyo basi ji ni mpana zaidi kuliko uvumishaji.

Asante kwa kutembelea Masshele blog 
+255766605392

MAREJELEO
Matinde, S.R (2012) Dafina ya lugha, Isimu na Nadharia, Mwanza: Serengeti Educational Publishers (T) Ltd
Habwe, J na Karanja, P, (2004). Misingi ya sarufi ya Kiswahili; Nairobi- Kenya: phoenix publishers Ltd