TABIA KUMI (10) AMBAZO WANAWAKE WENGI HUCHUKIZWA NAZO
TABIA 10 ZA WANAUME AMBAZO WANAWAKE WENGI HUCHUKIZWA NAZO 1. Kijana wa mama Mwanaume wa aina hii wakati wote utamkuta kagandana na mama yake katika kilakitu kuanzia maongezi hadi matendo, hawezi kufanya chochote mpaka apate idhini kutoka kwa mama yake hata kama ana mke na maamuzi yanayofanywa ni ya kuihusu familia yake yeye. Katika familia ya mwanaume huyu mama yake huwa ndiyo mfalme katika kila kitu, yeye ndo ataamua mkae wapi, mjenge wapi, muende wapi, mlenini, na hata maamuzi mengine mkiyaamua ninyi basi yeye ataulizwa na mtoto wake ayakague kama ni maamuzi sahihi au la, na mara zote maamuzi yake ndiyo ya mwisho. Kwa mwanaume kama huyu kama wewe ni mke basi ufahamu mapema kuwa hata ufanyaje kamwe huwezi kuwa mzuri na mwema kama mama yake. 2. Mwanaume mvivu na mchungu: Mwanaume wa jinsi hii ni kati ya wale ambao hawataki kabisa kujishuhulisha, wao hutaka kuwa na wanawake wenye kitu kama vile gari, nyumba, kazi nzuri n.k. utamkuta mwanaume wajinsi hii yeye ni kulala t...