Na
*Abdul Nondo*

Uchambuzi mfupi kwanini Godwin Mollel hatoshinda jimbo la Siha,isipokuwa kwa  nguvu na udanganyifu (election rigging)

Tuelewane kwa kitaalamu kabisa,kisayansi ya siasa kuna aina tatu zinazotumiwa na wananchi kupiga kura.

1. *party Identification model* hii ni aina ambayo mpiga kura humpigia mgombea wake sababu tuu,ni mgombea wa chama chake hivyo lazima ampigie.Tuelewe kuwa mkoa wa Kilimanjaro sio ngome ya CCM ,ile ni ngome ya Chadema ikiambatana na arusha hizi ni ngome za Chadema hivyo,watu ambao watampigia moleleli kwa misingi ya Chama cha CCM sio wengi,hivyo wengi sababu ni wanachama wa Chadema watampigia Elvis Christopher Mosi sababu ya misingi ya uchama kuwa ni kutoka chama chao.hivyo kwa sababu hii MOLLELI hana nafasi ya ushindi kwa kigezo hiki.sababu wanachama wa chadema Kilimanjaro na Siha,hadi maeneo ya Soweto,Longuo  kwa ujumla Chadema ni wengi zaidi ya CCM,pia tukumbuke hao hao CCM ambao ni wachache bado hawakubaliani na wamechafukwa na CCM kumsimamisha Molleli.

2.Aina nyingine ya kupiga kura ni *Sociological model* Hii ni aina ya upigaji kura ambayo watu wanamchagua mgombea kwa misingi ya ukabila(tribe,ethnics) au dini (religion),hata urafiki na mahusiano.hii upande wa Kilimanjaro hasa katika Jimbo la siha ni kubwa saana ,Jimbo la siha lina makabila kadhaa kabila kubwa ni *wasiha* ambao ndio wengi la pili ni wamasai ambao ni kabila la pili na makabila mengine yamechanganyika kutokana na shughuli za kiuchumi na kilimo,ambayo haya ni madogo madogo.

Moleli ni mmasai ,tukianza na kabila lake hadi sasa wamasai wamechafukwa sababu wanalalamika kuwa wamesalitiwa vikali na mollel,hivyo molleli kabila lake ambalo lingemuunga mkono limegawanyika hadi sasa.,pili upepo wa ushindi wa moleli 2015,ulivumwa na Edward Lowasa ndiye aliyemsaidia saana Molleli kushinda 2015. na taarifa nilizopata za ndani ni kuwa wamasai ndio walioandika barua kamati kuu ya CHADEMA kuwa CHADEMA wasiache kusimamisha mtu *Siha* sababu wamesalitiwa na Molleli. hawawezi mchagua tena.

Kabila lingine ni *wasiha*hawa wasiha ndio wengi walihitaji  *AGGREY MWANDRI* achukie fomu agombee tena ambaye ni msiha mwenzao lakini CCM wamepinga hilo sababu eti wamempa Mkuu wa mkoa wa Tabora,hivyo Wasiha wamechafukwa kwa CCM kumuweka Molleli ambaye hatakiwi hata na wamasai wenzake.

CHADEMA ikacheza vizuri hesabu zake,Ikamleta *Elvis Christopher Mosi* ambaye anatokea kabila la Wasiha,hivyo Wasiha wameridhishwa nae,pia wamasai wameridhishwa nae sababu walihitaji yeyote kutoka popote sio Moleli tena sababu amesaliti.pia makabila mengine madogo madogo wameridhishwa na Elvis Christopher Mosi sababu wamesalitiwa na moleli.

3. Aina nyingine ya upigaji kura kwa wananchi ni *RATIONAL CHOICE MODEL* hawa ni watu wanaochagua kuamini katika vigezo vya nani anafaa,nani jasiri,nani mkweli,nani anasifa,nani anaonesha dhahiri kwenda kuchochea maendeleo,nani anaenda kusaidia utatuzi wa shida zao,hili kundi ni la watu wenye kujielewa saana.

Hivyo kundi hili litatawaliwa na pre-conceptions (Maamuzi ,hukumu tangulizi)watakapopima sifa na vigezo nani anafaa ,watakuwa rahisi saana kuhukumu kwanza tofauti na kawaida yao,sababu ya maamuzi ya Molleli kujiengua katika ubunge bila sababu za msingi kundi hili ni rational, thinkers hivyo kujiengua kwa moleli kutawapa jibu wao moja kwa moja kuwa sifa na vigezo moleli hafai.

Hivyo kura yao itakuwa ni rahisi kumpigia *Evis Mosi* wa CHADEMA sababu yeye watapima Sera zake tuu,sababu ELVIS ndio Mara ya kwanza anaomba akatumikie.hivyo moleli atapoteza kirahisi saana.

Abdul Nondo.
0659366125
0762082783.
Abdulnondo10@gmail.com