Posts

Showing posts from October, 2017

Mtandao wa WhatsApp Waruhusu Kufuta Ujumbe

Image
  Ilishawahi kukutokea kutuma ujumbe, picha au video au documenti yeyote kwa mtu usiyemkusudia kwa bahati mbaya kupitia programu ya WhatsApp? kama huwa unapatwa na matatizo hayo sahau kabisa kwani tayari programu hiyo imeshaongeza sehemu ya kufuta jumbe hizo. WhatsApp is rolling out the Delete for Everyone (Recall) feature for all users! 🎉https://t.co/3bnbgxtPvU — WABetaInfo (@WABetaInfo) October 26, 2017 WhatsApp tayari imezindua huduma hiyo ambayo imeongezwa kwenye programu kwa jina ‘Delete For Everyone’ ambapo mtumaji wa ujumbe, picha au video atachagua kufuta kwake au kwa mtu aliyemtumia kimakosa. Kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwa watumiaji wote wa iOS na Android kama bado basi cha kufanya update programu yako ya WhatsApp ili uanze kutumia. Hii inakuwa hatua nyingine ya maboresho ya programu hiyo baada ya kutangaza kuongeza sehemu ya Live Chart  ndani ya mwaka huu. Mwanzoni mwa mwezi Agosti mwaka huu WhatsApp Inc walitangaza kuwa wataleta mabadiliko makub...

SIMBA WAMSHUTUMU REFA SASII KUWABEBA YANGA...WADAI ALIWANYIMA PENALTI MBILI ZA HALALI

Image
KLABU ya Simbe imelalamika kunyimwa penalti mbili na refa Heri Sasii katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC uliomalizika kwa sare ya 1-1 Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Sunday Manara amesema refa alikwenda na matokeo yake uwanjani.  Manara aliwawekea Waandishi wa Habari video ya mchezo huo kuwaonyesha namna ambavyo refa Sasii hakutoa penalti licha ya mpira kuwagonga mikononi beki, Kevin Yondan na kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi Jumamosi. Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi (kushoto) akizungumza na refa Heri Sasii (kulia) Jumamosi Manara aliyewabeza watani wao hao wa jadi, kwamba ni kawaida yao kupendelewa na marefa kila wanapokutana na Simba amesema watapeleka malalamiko Bodi ya Ligi dhidi ya refa huyo na wengine walioionea timu yao katika mechi zilizotan...

900 wasimamishwa shule, kisa binti mmoja

Image
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, karibu wanafunzi 900 wa Shule ya Sekondari Kabale katika Manispaa ya Kabala nchini Uganda wamesimamishwa masomo kutokana na vurugu kubwa zilizoibuka shuleni hapo, chanzo kikielezwa ni kumgombea kimapenzi binti mmoja ambaye pia ni mwanafunzi shuleni hapo. Wanafunzi hao waliibua vurugu kubwa na kuanza kupigana mchana wa Ijumaa iliyopita shuleni hapo. Inaelezwa kuwa, mwanafunzi wa kidato cha sita aliomba kuwa na uhusiano na binti ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi mwingine wa kidato cha nne. Kutokana na kuvuja kwa taarifa hizo, makundi mawili ya wavulana hao yaliibua uhasama ulioishia kupigana. Ugomvi huo haukuishia kwa wanafunzi tu, waliharibu pia mali za shule na hata za majirani wanaoishi karibu na shule hiyo. Kutokana na hali hiyo, jeshi la Polisi lililazimika kuingilia kati kutuliza ghasia kwa kutumia mabomu ya machozi na silaha nyingine kutawanya wanafunzi hao. Kaimu Ofisa anayeshughulikia usalama wilayani Kabale, ...

Nafasi za kazi leo October 31

Image
Bonyeza Link zifuatazo Kusoma na Kuapply: 7 Job Opportunities at TANROADS Tanzania 5 Job Opportunities at Fastlink Safaris & Tours Limited, Sales and Marketing Personnels Job Opportunity at Trade Mark East Africa Job Opportunity at South Beach Resort, Female Receptionist 2 Job Opportunities at Hallmark Attorneys Job Opportunity at Zanzibar White Sand Luxury Villas Job at Tala, Operations Manager Job at UN Women, National Consultant Job Opportunity at KaziniKwetu, Sales Representative Job Opportunity at KaziniKwetu Ltd, HSE Officer Job Opportunity at KaziniKwetu Ltd, Electrical Engineer Nafasi zingine zaidi ingia www.ajirayako.co.tz

Kiongozi wa Catalonia aliyefutwa "aenda Ubelgiji"

Image
  Rais wa Catalonia aliyefutwa Carles Puigdemont ameenda nchini Ubelgiji, wakili wake aliye chini humo anasema. Wakili huyo Paul Bekaert, hakuzungumzia ripoti kuwa Bw. Puigdemont anajiandaa kuomba kupewa hifadhi. Mwendesha mashtaka nchini Uhispania ametaka mashataka ya uasi kufunguliwa dhidi yake na viongozi wengine ya kura ya maoni iliyopogwa marufuku. Serikali ya Uhispania ilichukua udhibiti kamili wa Catalonia siku ya Jumatatu, kuchukua mahala pa viongozi waliofutwa. Ilifuta utawala wa eneo hilo na kuitisha uchaguguzi mpya baada ya Bw Puigdemont na serikali yake kujitangazia uhuru wiki iliyopita. Wakili huyo wa Ubelgiji Paul Bekaert alisema kuwa Bw. Puigdemont kwa sasa yuko mji mkuu wa Ubelgiji Brussels. Mbona Puigdemont akaenda Ubelgiji? Uhispania ilikuwa imekumbwa na mzozo wa kikatiba tangu kura ya maoni iliyopangwa na serikali ya Bw. Puigdemont, ilipoandaliwa tarehe mosi Oktoba kinyume na amri ya mahakama iliyoamua kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na katiba. Serik...

TAARIFA YAKUJIUNGA NA JKT

Image
TAARIFA KWA UMMA Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo anawatangazia vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea mwaka 2017. Utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo, unaratibiwa na ofisi za Wakuu wa mikoa na wilaya ambapo muombaji anaishi. Zoezi la kuchagua vijana litaanza Mwezi Novemba 2017 na vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 04 mpaka 09 Desemba 2017. Jeshi la Kujenga Taifa linaendelea kusisitiza kuwa nafasi za vijana kujiunga na mafunzo ya JKT haziuzwi, aidha yeyote atakaye husika na utapeli wa kuuza au kununua nafasi hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria. Sifa za mwombaji ni kama ifuatavyo: Awe raia wa Tanzania. Kwa vijana wenye elimu ya Darasa la Saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18. Vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne ni kuanzia miaka 18 hadi 2...

Makosa Mawili anayotuhumiwa kutenda Zitto Kabwe

Image
  Upadates Kutoka Kituo cha Polisi Chang'ombe, mkoa wa kipolisi Temeke, Dar es salaam anakoshikiliwa Zitto Kabwe Kwamujibu wa taarifa kutoka kwenye kamati a sheria na katiba ya chama hicho, imeeleza kuwa Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe, amekamatwa na polisi na kuhojiwa akituhumiwa kufanya makosa ya Uchochezi. Kwamba juzi, Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke alitoa maneno yanayoweza kupelekea uvunjifu wa amani. Maneno hayo ni yafuatayo: 1. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo. 2. Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwe...

Picha & Video : MBUZI ANAYEFANANA NA BINADAMU AZALIWA MBARALI MBEYA ASUBUHI HII

Image
Wakazi wa kijiji cha Igurusi kata ya Igurusi tarafa ya Ilongo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wamepigwa butwaa baada ya mbuzi aliyepo katika kijiji hicho kuzaa mtoto anayefanana na binadamu kama unavyoona kwenye picha. Tukio hilo limetokea leo Jumanne Oktoba 31,2017 majira ya saa 2 asubuhi, nyumbani kwa mkazi wa kijiji hicho maarufu Mwakasinga. Muonekano wa mbuzi anayefanana na binadamu -  Picha kwahisani ya  John Robert - Malunde1 blog TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

Yanga kumaliza hasira zao kwa Singida United.

Image
KOCHA WA TIMU HIYO, GEORGE LWANDAMINA. BAADA ya kuambulia pointi moja dhidi ya Simba kwenye mechi iliyopita katika Uwanja wa Uhuru, Yanga itaondoka Dar es Salaam kesho kuelekea Singida ikiwa na hasira ya kukisambaratisha kikosi cha Hans van der Pluijm, Singida United. Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, kama ilivyo kwa Singida United na Simba, Jumamosi ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya watani zao hao wa jadi kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara. Kikosi hicho cha Yanga katika safari hiyo, kitaendelea kuikosa huduma ya wachezaji wake wa kigeni, Amissi Tambwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko ambao bado hawajapona kwa asilimia 100. Akizungumza na Nipashe jana, kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, alisema kuwa matokeo waliyoyapata dhidi ya Simba yamewapa ari ya kufanya vizuri kwenye mchezo wao huo wa ugenini. "Hatutakuwa na Tambwe, Ngoma na Kamusoko kama ilivyokuwa kwenye mchezo dhidi ya Simba, lakini hilo halinipi shida sana,...

VIFARANGA 6,400 KUCHOMWA MOTO ARUSHA

Image
  Arusha. Vifaranga vya kuku 6,400 vinatarajiwa kuchomwa moto baada ya kunaswa vikiingizwa nchini kupitia Longido mkoani Arusha. Vifaranga hivyo vilikamatwa juzi vikitokea nchini Kenya. Taarifa zinasema thamani ya vifaranga hivyo ni Sh12.5 milioni na ni mali ya mfanyabiashara Mary Matia (23) mkazi wa Mianzini jijini Arusha anayeshikiliwa na polisi. Akizungumza na Mwananchi katika mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Namanga, ofisa mfawidhi wa Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa ya Mifugo Kanda ya Kaskazini, Obedi Nyasembwa alisema tangu mwaka 2007 Serikali ilipiga marufuku kuingiza mayai na vifaranga kutoka nje ya nchi. Alisema uamuzi huo wa Serikali ulichukuliwa ili kudhibiti magonjwa ya mifugo ukiwamo wa mafua ya ndege. “Kwa mujibu wa Sheria ya Magonjwa ya Wanyama ya mwaka 2003, vifaranga hivi tutaviteketeza kwa kuwa vinaweza kuwa na magonjwa,” alisema. Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpaka wa Namanga, Edwin Iwato alisema kwa mujibu wa sheria...

Sababu za Rais Magufuli Kutokugawa Milion 50 Alizoahidi Kwa Kila Kijiji

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ameeleza sababu zinazomfanya achelewe kutimiza ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji alizoziajidi wakati wa kampeni za kugombea urais kuwa ni kutokana na kuwepo kwa mambo mengi nchini yanayohitaji utekelezaji wa haraka. Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika mkutano wa hadhara ikiwa ni moja ya vitu alivyopanga kuvifanya katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani hapo. Ameeleza kuwa ameona ni sahihi kuanza na mambo ya muhimu zaidi kama vile miundombinu ya barabara, huduma za afya pamoja na elimu kabla ya kutoa fedha hizo ambazo aliziahidi katika iilani ya uchaguzi wa mwaka 2015. “Halitokuwa jambo jema mimi kutoa milioni 50 kwa kila kijiji nchini wakati huduma mbalimbali kama vile elimu, afya na miundombinu ya barabara na usafirishaji haijakaa vizuri. lakini niwahakikishie kuwa hizo fedha zipo na zitakabidhiwa kwa kila kijiji kama nilivyosema,...

Burnley waipiga Newcastle 1-0

Image
Burnley: Pope, Lowton, Tarkowski, Mee, Ward, Brady, Defour (Westwood 76), Cork, Gudmundsson, Hendrick, Barnes Subs not used: Vokes, Wells, Lindegaard, Bardsley, Long, Arfield Goalscorers: Hendrick 74  Booked: Gudmundsson, Cork, Tarkowski  Newcastle: Elliot, Yedlin, Lascelles, Lejeune, Manquillo, Diame (Gayle 83), Shelvey, Ritchie (Murphy 79), Perez (Hayden 76), Atsu, Joselu Subs not used: Clark, Saivet, Darlow, Jesus Gamez Referee: Mike Dean

Kufanya mapenzi mara kwa mara kunaboresha afya yako

Image
Kufanya mapenzi ni mojawapo ya vitu vichache ambavyo watafiti wanasema vinamfanya mtu aburudike huku mwili wake ukifaidika kutokana na tendo hilo. Utafiti umeonyesha kwamba kufanya tendo la ndoa mara kwa mara kunatibu mafua, kuepusha magonjwa ya moyo, kunazuia kansa na hata kuongeza urefu wa maisha. Watafiti katika chuo kikuu cha Nottingham University nchini Uingereza wamegundua kwamba wanaume wenye umri zaidi ya miaka 50 wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara wana uwezekano mdogo sana wa kupata kansa ya kibofu. Watafiti hao walikanusha madai kwamba kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara 20 kwa mwezi kunaongeza uwezekano wa kupata matatizo ya moyo. Madaktari wamekubaliana kwamba mapenzi ni kama shughuli zingine za kawaida na ni mazoezi bora kwa afya. "Kwa kulinganisha na mazoezi, kufanya mapenzi ni sawa na kutembea zaidi ya kilomita moja au kupanda na kushuka ngazi za majengo mawili marefu" alisema Dr Graham Jackson wa hospitali ya St Thomas. Utafiti uliofanywa ...

BREAKING: Zitto Kabwe akamatwa na Polisi asubuhi hii

Image
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa asubuhi hii na Afisa Habari wa Chama hicho Bwana Abdallah Khamis imeeleza kuwa KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo,Zitto Kabwe,amekamatwa na jeshi la Polisi muda huu akiwa nyumbani kwake na anapelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe Sababu za kukamatwa kwake ni hotuba ya juzi Oktoba 29, 2017 katika kata ya Kijichi, Mbagala Jijini Dar es salaam katika uzibduzi wa kampeni za uchaguzi wa mdogo wa madiwani kwenye kata 43 nchini

Irene Uwoya afunga ndoa na Dogo Janja

    Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi juu ya tetesi iliyopo mtaani kuhusu kuolewa na msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja na kusema ni kweli ameolewa na msanii huyo kwani ndiye mwanaume wa ndoto yake. Irene Uwoya kupitia mtandao wake wa Instagram amethibitisha hilo na kusema kuwa anampenda sana msanii huyo na kudai huyo ndiye mwanaume wa ndoto yake hivyo anafurahi kuona wamefunga pingu ya maisha.   "Nimeolewa na mwanaume wa ndoto zangu, bado naendelea kulia na kutokwa na machozi ya kwa furaha. Dogo Janja nakupenda sana na nimefurahi kumaliza maisha yangu ya duniani nikiwa na wewe" aliandika Irene Uwoya. Kufuatia ujumbe huu ni wazi kuwa Irene Uwoya atakuwa amejibu maswali ya watu wengi ambao walikuwa hawaelewi nini kinaendelea kufuatia tetesi kuwa watu hao wamefunga ndoa siku za karibuni.

Lowassa amkaribisha Nyarandu Chadema

Image
  Dar es Salaam: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua nyadhifa zote alizokuwa nazo CCM. Akionyesha kuwa na furaha alipozungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”. Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango. Dakika chache tangu Nyalandu aombe kujiunga na Chadema, Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani. “Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne. “Nyalandu ni hazina, ni mbunge imara na ni mwanasiasa ...