Njia za kufanikiwa katika Betting




Watu wengi wanachukulia mchezo wa kubashiri matokeo (betting) kama ni mchezo usiofaa katika jamii, lakini mimi napingana na huo mtazamo ambao upo kwa watu wengi. Kwa namna nyingine huu mchezo unategemeana na wewe mchezaji unavyouchukulia na namna unavyoshiriki kuucheza. Kimsingi kama ukiuchukulia huu mchezo kama ndio chanzo chako cha kupatia kipato na ukaucheza bila staha ukitegemea utaenda wewe unavyofikiri au unavyotaka na matokeo yake ikawa tofauti unaweza kuuchukia huu mchezo na kuuona mbaya sana. 

Huu mchezo ukiuchukulia staha na kuucheza kwa makini ni mchezo unaoweza kuwa msaada katika maisha yako hasa kukusaidia kuinua kipato chao.

JARIBU KUFUATA HIZI NJIA ILI KUWEZA KUFANIKIWA KATIKA BETTING
  1. Usiufanye huu mchezo wa kubet kama chanzo chako kikuu cha mapato cha kutegemea. Hii itakuepusha wewe kutoshusha kipato chako hata iwapo hutapata matokeo uliyotarajia katika betting.
  2. Ukizingatia ya kwamba huu ni mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali usiwe unategemea matokeo ya upande mmoja tu, tegemea ya kwamba matokeo yoyote yanaweza tokea hata kinyume na matarajio yako. Hii itakupunguzia mfadhaiko pindi mambo yanavyoenda ndivyo sivyo.
  3. Kamwe usipende kutumia fedha zako za mambo ya muhimu katika mchezo huu (mfano fedha za kuendesha maisha yako na familia kila siku). Tumia fedha za ziada unazozipata, kwa mfano zile ambazo ungeweza kunywa bia na marafiki zako. Hii itakusaidia wewe kuendelea na maisha yako kama kawaida endapo mambo yataenda ndivyo sivyo katika betting.
  4. Jaribu kufuatilia kwa ukaribu michezo unayopenda kubashiri, hii itakusaidia kupunguza uwezekano wa kupoteza mara kwa mara kwani utakuwa angalau unazijua timu unazobashiri uwezo wake. Unaweza kufuatilia kujua pia ligi cha nchi mbalimbali kujua huwa zinapenda kutoa matokeo ya namna gani, hii itakusaidia namna ya kuchagua betting zako kwani kuna option nyingi. Kwa mfano unawezajua timu za mpira wa miguu A na B huwa zikutana lazima kadi nyekundu iwepo kwa hiyo unaweza bet mechi ya leo kadi nyekundu itakuwepo. Au timu D na C huwa zinafungana magoli mengi kwahiyo ukaamua kubet labda mechi ya leo itakuwa na jumla ya magoli 3 au 4 nakuendelea.
  5. Cheza kwa kiasi mchezo huu. Usiwe na tamaa kwamba unaweza pata pesa nyingi kwa mara moja kwahiyo ukacheza hovyo bila mpangilio, hutaumia. Jaribu kuweka mikakati na mipangilio juu ya uchezaji wako, hakika hutajuta. Cheza mechi chache kwa siku unazoamini zinaweza kukupatia ushindi sio lazima ubashiri mechi nyingi kwa mkupuo. Hii itakusaidia wewe kukupa ushindi mara nyingi.
  6. Usibashiri kwa mapenzi ama ushabiki, eti kwa kuwa mimi ni mshabiki wa Azam Fc sasa ndo nakuwa naitabiria ushindi kila mara, angalia uwezo wa timu yako dhidi ya timu pinzani kama inaweza shinda na hii itakuwa rahisi endapo utakuwa mfuatiliaji mzuri pia wa ligi ama mchezo unaobashiri.
  7. Usiuchukulie serious sana huu mchezo na wala usiruhusu ukutawale sana ufanye kama ziada hakika utaufurahia.
Ni hayo tu kwa leo wandugu tutazidi kujuzana mengineyo mbele ya safari yetu 

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?