KOSA SI KIDONDA

Kukosea kumekuwa ni sehemu ya kila kiumbe duniani. Kuanzia unapozaliwa  ni mara nyingi Sana'a utajikuta kwenye makosa aidha kwa kujua ama kwa kutokujua. Pamoja na kuwa ni asili ya mwanadamu kukosea jambo hili limekuwa na uzito mkubwa sanaa kwenye maisha yetu na hii ni kwa kuwa watu wengi huona makosa zaidi kuliko mema au mazuri atakayofanya mwingine.
Kukosea kumefanya watu kujidharau na kurudi nyuma katika hatua zao. Naamini utakubaliana nami kuwa ni Mara nyingi tumekuwa tukijuta na kuumia na wengine hata kulia tukikumbuka Yale tuliyoyafanya nyuma. Lakini umeshawahi kujiuliza baada ya uchungu huo na maumivu ni nini kitafata!??
Je utaendelea kulia kila siku na kuumia na kuishi maisha ya kujilaumu kwa makosa yako??!!
Je kitabadilika nini baada ya majuto hayo ??  
Jibu la haraka ni kuwa hakuna kitakachobadilika na hapa ndio nakumbuka ule msemo wa Yaliyopita si ndwele tugange yajayo 
Ni lazima Leo  uamue kuishi maisha mapya ,kukubali kuwa MTU mpya, kufanya mambo mapya na kuchukua hatua nyingine 
Usikubali kurudi nyuma, USIJILAUMU, USILIE, USIJUTE kwa yaliyotokea usikubali maisha yako ya sasa yalinganishwe na Yale ya Jana.
JISAMEHE, SIMAMA, ANZA hatua mpya Leo. 
Kubali kujifunza kwa Yale uliyokosea lakini kamwe usikubali makosa yako yaharibu maisha yako ya sasa au yakufanye uonekane MTU mbaya.
Kumbuka KUTELEZA si KUANGUKA.  Kila siku ujiambie LEO NIMEKUWA BORA ZAIDI YA JANA na Kuanguka kumenifundisha kusimama.

Comments

  1. Jisamehe, Simama anza Upya leo. Hakika kweli leo nimejifunza kitu kikubwa sana maishani mwangu.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?