Hatimaye Denti UDSM Aliyeuawa na Polisi kwa ‘Ujambazi’ Azikwa Kisutu, Dar
Hatimaye Denti UDSM Aliyeuawa na Polisi kwa ‘Ujambazi’ Azikwa Kisutu, Dar
Mwili wa denti wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Marehemu Salum Almas aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi kwa madai kuwa alikuwa Jambazi, Mei 14, mwaka huu maeneo ya Uhamiaji Kurasini jijini Dar, ukiwa umebebwa tayari kwa kuzikwa katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar.
TAZAMA MAZISHI HAYO
Mwili wa Denti huyo wa UDSM uligomewa kuzikwa na ndugu zake kwa madai kuwa aliuawa kimakosa kwa kudhaniwa ni jambazi aliyetaka kupora fedha kwenye ATM iliyopo maeneo ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar.
Mwili wa Marehemu uliswaliwa katika Msikiti wa Kichangani, Magomeni, Dar mara baada ya swala ya Ijumaa. Hapa chini nimekuwekea picha 12 za msafara kuelekea makaburini.
(STORI: BONIPHACE NGUMIJE, GLOBAL TV ONLINE)
Comments
Post a Comment