Kama hukusikia hiki kihoja soma hapa
SIKU FIDEL CASTRO ALIPOMUKABA NYERERE TAI AIRPORT DAR ES SALAAM!!
kwanini alimukaba?? fuatana nami. Ilikuwa ni mwaka 1982, ilikuwa ni ktk mapokezi ya viongozi wa nchi zilizofuata siasa za mlengo wa kushoto. Yahaani nchi zilizofuata siasa za Max!! siasa za usoshalisti (UJAMAA) zikiongozwa na UNITED SOCIALISIT SOVIET UNION au URUSI, kisha Uchina ya Mao tise dong, Cuba, Venezuela, Northern Korea, Romania, Tanzania n. k. Mkutano ulifanyika Dar es salaam ktk ukumbi wa Karimujee.
Kambarage alikuwa airport akiwapokea viongozi hao, kisha transport officer wa ikulu alikuwa na kibarua cha kusafirisha hadi kwenye mahoteli walikopangiwa kufikia, wapo waliofikia Sea cliff. hotel, wapo waliofikia Peacock hotel, wapo waliofikia Sheraton hotel, na kwingineko!! Mara akateremka Comrade Fidel Castro kwenye ndege, ndege haijasimama yeye keshafungua mlango na kudondoka nje yupo anaturoti. Wahuni Dar es salaam nao hawakukawia kumushangilia kwa kelele na vigelele!! Mtangazaji airport naye hakusau jukumu lake la kutangaza majina ya viongozi wanaotua, vipaza sauti navyo vikamtii Mtangazaji "" huyo ni Mh Fidel Castro Rais wa Cuba aliyekwenda kupindua nchi akiwa amepanda juu ya mgongo wa mamba akitokea pwani ya Miami kule Marekani "Mtu mwenye UWEZO tangu utoto wake" "aliongeza Mtangazaji!! navyo vifijo vikaongezeka, wahuni wakaanza kupiga sambasoti mbele ya Nyerere
Mara miamba hii miwili iliyoigawa dunia kwa sera ya siasa za kutofungamana na upande wowote ikakutana ili kusalimiana. Alikuwa ni Rais Nyerere aliyetangulia kumpa Castro mkono, Castro akaupokea mkono wa mwalimu kwa kuutikisa kwa nguvu akiashilia wanaume wamekutana !! Mara wakaangukana vifuani ili kukumbatiana, katika kukumbatiana ndipo Fidel Castro akagundua kuwa Mwalimu alikuwa hajavaa bulletproof ile jacket yakuzuia risasi.
Castro akashangaa sana!! kisha akasema "" Mr president, you don't wears a bulletproof?? this is the wrong mistake!! "akimanisha mr president, huvai umbulletproof ili ni kosa kubwa!! Usijali mr Castro, hii ni nchi ya amani!" Nyerere alijibu. Nchi ya amani?? Je, wakikushoot risasi ya kifuani?? "aliuliza Castro. Hapana hii ni nchi ya amani, peaceland,,,,,.." alijibu mwalimu. Nchi ya amani,,?? "wewe ni amiri jeshi, acha mzaha na uhai Kambarage" "alisema Castro huku akiwa amemkaba kala za gwanda zito la kijani alilopenda kuvaa mwalimu!! Ma bodyguards wa Mwalimu walibaki wakimtumbulia Castro macho!! Huku Kambarage akicheka. Mara Castro akapelekwa kwa mwalimu pale Msasani, ndipo Castro akaonyesha kitimbwi kingine, kabla ya kuingia ndani Castro akasema "" Mr president I want your security men to check me as common please!! "" akimanisha akaguliwe kabla ya kuingia ndani!! Askari wane walimukagua kwa zamu na kudai hana silaha yoyote!!!! Mr president maafisa usalama wako wote wameisha???aliuliza Castro. "" Hapana!!! amebaki kijana mmoja, "" alijibu Kambarage, "basi mwiteni alisema Castro. Kijana aliyeitwa alikuwa ni Luteni Tamimu, sasa ni marehemu, Tamimu alikuwa amechukua diploma yake ya ulinzi nchini Cuba, huyu Luteni Tamimu alikuwa ni miongoni mwa Vijana wa UMMA PARTY waliokuwa wamechukuliwa Cuba kusoma na Abdurahiman Babu ili waje waongoze mapinduzi matukufu ya ZANZIBAR ya January 12 /1964. Babu naye sasa amelala tayari. Tamimu kufika akachukua vishikizo vya combat la Castro akaving'oa na kisha kuvishikamanisha ikawa bastola, kisha Tamimu akamukabidhi Nyerere kwa kusema, "mzee hii ni silaha tosha, mwalimu akatabasamu. Ndipo Castro aliposhindwa kuuficha hisia zake mbele ya mwalimu wa Walimu." unaonaje Mr president unipe huyu askari mmoja mimi nikupe mgambo 40? aliomba Castro. "" No!! no! no!! it is impossible!! "alijibu Kambarage akimanisha haiwezekani. Tamimu baadae alikuja akauawa kwa risasi kutokana na msako wa polisi jamii baada ya kutafutwa kwa kipindi kirefu na polisi kutokana na TUHUMA za uhaini. Askari walipoingia kwake upanga Tamimu aliruka ukuta wa geti kisha akatokea NG'AMBO ya pili, kule nako akaruka geti la wahindi na kutokea upande wa pili wa barabara,. Mda huo wote alizidi kukimbizwa na kikosi maalumu cha askari waliopata mafunzo Urusi. Kuona hivyo akadandia gari moja la kusambaza bia, kisha akaanza kuwashambulia askari polisi kwa chupa za bia. Marehemu Tamimu alikuwa anaichukua chupa ya bia anaitikisa na kisha anawatumia askari. Basi chupa inalia kama mzinga!! Ndipo askari mmoja alipomuhesabu risasi ya bega karibu na moyo, risasi ile ilimpata na kumurusha kama swala!! ukawa ndio mwisho wa Tamimu. Castro alipojua alikasirika na kusema msingemuua, mugemleta hata huku.
Mkutano uliendelea pale Karimujee hall!! Castro hakuacha vituko!! mara ghafla kwenye usiku wa saa tatu unusu umeme ukakatika ghafla ukumbini na giza likatawala, inasemekana baada ya sekunde kama kumi na mbili hivi umeme ukarudi ghafla!! Mara wakamuona Fidel Castro akishuka kutoka kwenye paa la ukumbi na kutua palepale kwenye kiti chake kama nyani. Marais wenzie kumuuliza kulikoni, Castro anajibu " Hayo ni machale tuu yalinicheza" mkutano uliisha na Fidel alirudi nyumbani. Inasemekana babake Castro, yahaani mzee Castro Ruiz alikuwa ni mu America lakini mama ni Muyahudi. Wale wayahudi waliotangatanga duniani enzi za Adolf Hitler!!
Fidel Castro aliingia madarakani baada ya kuongoza mapinduzi yaliyomung'oa mtawala wa kisiwa hicho dikiteta Fulugensio Batista mwaka 1959. Alianzia mapambano visiwa vya Mayari hukohuko Cuba. Inasemekana waliompa silaha na pesa za za kupindulia nchi walikuwa ni Wamarekani na Waingereza ili baadae Cuba iwe himaya ya Waamerica, lakini Castro walichomutuma sicho alichokifanya. Baada ya kupindua akawageuka. Kwamba mimi ndiye President, hivyo sielewi cha Mumarekani wala Mwiingereza, alisababisha uhasama mkubwa uliodumu mpaka leo!!
Ujanani Castro aliwahi kuuza shamba lake huko kijijini na vifaa vyote hadi kitanda yeye na mdogo wake Raul Castro ili kuwanunulia bunduki rafiki zao 150 waunde jeshi la siri. Kisha wakaanza kulala kwenye carpet yeye na mke wake Natasha Castro na kuishi maisha ya kushindia kahawa. Hiyo mbinu haikufaulu, walizimwa vikali na jeshi imara la mfalme Fulugensio Batista mwaka 1948. Ujanani pia Castro aliwahi kugombea kiti cha uraisi akapata asilimia mbili tuu ya kura zilizopigwa, yeye akadai amefurahishwa na matokeo hayo. Wakati huo alikuwa na umuri wa miaka 24 tuu!! CASTRO ndiye askari mmoja tuu duniani aliyekuwa na uwezo wa kuandika jina lake kwa kupiga risasi angani usiku na ule mwanga wa risasi unaandika jina FIDEL CASTRO RUIZ!! Lakini pia CASTRO ndiye Rais wa pili duniani tangu mwanzo wa dunia kusimama masaa mengi jukwaani huku akihutubia!! Wa kwanza alikuwa ni Adolf Hitler yeye alisimama masaa 72, akiangalia askari watakaokwenda kupigana vita ya kwanza ya dunia, pasipo kutoka wala kwenda kukojoa. Wa pili ni Castro mwenyewe, yeye alikuwa ana uwezo wa kusimama jukwaani masaa 12 "bila kuchoka, na akitoa kitabu cha hotuba zake huwezi kukibeba mkononi lazima ukifunge kwenye baiskeli. Wa tatu ni Sadam Hussein yeye alisimama jukwaani masaa manane.
Cuba Castro amefuta kabisa UJINGA UMASIKINI NA MARADHI!!! kazi ya chini kabisa kule Cuba, yahaani ile kazi ya aibu, ya kufanya ukiwa umejificha kwamba washikaji wakijua watani CHEKA ni kazi ya UDEREVA TAX!!! elimu ya chini kabisa ni degree moja, bachelor!! Kama hujamaliza degree moja, Cuba wanakusaka kama mtoto aliyetoroka shule ya msingi!! Wastani wa watu kuishi ni miaka 120, lakini wanataka kuiongeza ifikie 150 kama Japan!! Cuba ndiyo nchi pekee duniani ambayo kila raia wake anapoamuka asubuhi anajua atafanya nini, atakula nini na atalala wapi. Lakini pia Tanzania kweli ni nchi ya amani hata Clinton alikubali mwaka 1998, Clinton yeye alisema kuna kitu kilipandikizwa sio bure, alipotua nigeri na Uganda alilindwa kwa silaha nzito nzito za kisasa, akashangaa kufika Arusha kuna mgambo na rungu hata upinde na mishale hawana, eti taifa la AMANI Clinton alichoka!!
Comments
Post a Comment