Posts

Showing posts from December, 2016

Maskini, TANZIA habari mbaya watoto wa mchezaji wa simba waaga dunia

Image
Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya msiba wa watoto wa mchezaji wetu Juuko Murshid vilivyotokea leo huko kwao nchini Uganda. Vifo vya watoto hao watatu vimekuja katika kipindi hiki ambapo mchezaji wetu huyo wa kimataifa, akiwa kwenye maandalizi ya fainali za mashindano ya Afcon, yanayotarajia kuanza katikati ya mwezi ujao. Tunajua uzito wa kufiwa na watoto hao, na tunatambua uchungu alionao nyota wetu huyo, yeye pamoja na mkewe, lakini tunaamini Mungu atawapa subira na uvumilivu mkubwa katika kipindi hiki kigumu wanachopitia. Mwisho klabu inawatakia Wanasimba na Watanzania wote heri ya mwaka mpya 2017. Imetolewa na. *Haji S Manara* Mkuu wa Habari wa Simba SC. Comments

UHAKIKI RIWAYA MZINGILE

Image
UCHAMBUZI WA FANI KATIKA RIWAYA YA MZINGILE MBINU ZA KIFANI KATIKA RIWAYA YA MZINGILE YA E.KEZILAHABI (1991) Riwaya ya Mzingile ni riwaya ya kifalsafa iliyojikita katika swali “nini maana ya maisha Katika kujibu swali hili mwandishi amemtumia Kakulu aliyezaliwa katika mazingira ya ajabu kwa kumchora kama neema kwa maana ya kuona kama mkombozi kwa kutatua matatizo ya njaa na magonjwa. Hata hivyo Kakuru anapoteza maana baada ya watu kuanza kumpinga hivyo anakimbilia mlimani. Pia kwa kutumia swali nini maana ya maisha mwandishi anamlika taasisi za dini ambazo kimsingi ndio mhimili wa maadili zinaposhindwa kudhibitisha hilo kwa viongozi wa dini (mashekhe na mapadri) wanavyokiuka maadili. Kwa kutumia swali hilohilo pia mwandishi anaainisha matatizo yanayotokana na uongozi mbaya unaofanywa na viongozi wabadhilifu na wasiojali maslahi ya wengi, japo wananchi waliwaamini kwa kuwapa fursa hiyo kuongoza.Mwandishi amemaliza kwa kueleza kuwa jamii mpya iliyokuwa na unyanyasaji, utabaka na vitu v...

hadithi ya kusisimua

Image
UMESOMA HADITHI NYINGI ZA MAPENZI, LAKINI HII ITAKUSISIMUA KULIKO ZOTE, UTATUMIA DAKIKA 2 KUSOMA LAKINI... 1st year nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo. Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why 2nd year Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,n...

hadithi ya kusisimua

Image
UMESOMA HADITHI NYINGI ZA MAPENZI, LAKINI HII ITAKUSISIMUA KULIKO ZOTE, UTATUMIA DAKIKA 2 KUSOMA LAKINI... 1st year nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo. Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why 2nd year Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,n...

ATHARI YA MAJINA KATIKA MAISHA YA BINADAMU

Image
 Majina yana umuhimu na athari kubwa katika maisha ya mwanadamu. Ukimchagulia jina baya mtoto wako jina hilo linaweza kumfanya awe • Mwehu • Muhuni • Mlevi • Mpenda starehe • Mwizi na kadhalika Ukimchagulia mtoto wako jina nzuri linaweza kumfanya awe • Mpole • Mwenye heshima • Mcha mungu • Mwerevu • Mbunifu • Mtiifu • Mwenye Imani na kadhalika AINA YA MAJINA Kuna aina nyingi ya majina mfano:- • Jina la kuzaliwa • Jina la kubandikwa au la utani • Jina la umaarufu JINA LA KUZALIWA Ni jina ambalo mtu hupewa baada ya kuzaliwa watu wengi hutumia jina hili kwa maisha yake yote. JINA LA UTANI Ni jina ambalo mtu upewa kutokana na mambo yafuatayo:- MAUMBILE Ukiwa mfupi sana, mrefu sana, mwembamba sana, mnene sana au pia ukiwa mlemavu unaweza kubandikwa jina la utani. TABIA Ukiwa na tabia mbaya kama vile mwizi, mlevi, mzinzi, msengenyaji, kuomba omba pia watu wanaweza kukupa jina la utani. Ukiwa na tabia nzuri sana kama vile mkarimu, mtoaji, muucha mungu watu pia wanaweza kukupa jina la utani. ...

KUMBE BABU FERGUSON ANAMPA MORINHO SIRI YA USHINDI MAN U

Image
MANCHESTER, England KAMA ulikuwa unajiuliza na unakosa majibu juu ya nini kimeibadilisha Manchester United haraka hadi kuwa inatoa vichapo mfululizo, Mreno Jose Mourinho ameamua kufunguka na kuweka kila kitu hadharani. Mourinho amefichua kuwa Sir Alex Ferguson amekuwa akitembelea mara kwa mara kwenye mazoezi ya Manchester United katika viwanja vya Carrington. Hii ni mara ya kwanza kwa Ferguson (74) kutembelea kwenye mazoezi ya United tangu alipostaafu kuifundisha timu hiyo mwaka 2013 na kupewa cheo cha Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo. Ferguson ambaye amedumu United kwa miaka 26, alikuwa akifuatilia mechi tu za United na kutojihusisha na jambo lolote la kiufundi kwa takribani miaka mitatu sasa. Lakini Mourinho aligundua kuwa anamhitaji zaidi mkongwe huyo kwenye mipango yake hivyo kumwalika kwenye mazoezi na kumpa muda wa kuzungumza na wachezaji juu ya historia ya klabu hiyo. Akizungumza na mtandao wa United, Mourinho alisema: “Hakuwahi kufika hapa tangu alipostaafu lakini nimeamua ku...

NYOKA WA MAAJABU ALIVYO KUFA NA MTU WAKE

Image
DUNIANI kuna mambo, ndivyo unaweza kusema kutokana na mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) kufa baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi. Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo. Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka. Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku ame...

UHAHIKIKI RIWAYA YA MIRATHI YA HATARI

Image
 FASIHI YA KISWAHILI JIFUNZE FASIHI YA KISWAHILI KUTOKA KWA MWALIMU MWINCHANDE Tuesday, April 26, 2016 UHAKIKI WA RIWAYA YA MIRATHI YA HATARI KWA KUTUMIA FALSAFA YA KIAFRIKA Maana ya falsafa ya kiafrika kwa mujibu wa Placide Tempels, Falsafa ya kiafrika ni ile falsafa inayowashughulisha waafrika wenyewe na watu wengine ambao sio waafrika lakini wanakubaliana na mila, tamaduni za waafrika na fasihi simulizi za kiafrika.Hivyo falsafa ya kiafrika ni ile falsafa ambayo imejikita katika mifumo ya kijamii, mila na desturi na fasihi simulizi za kiafrika. Placide Tempels alizaliwa tarehe 18/02/1906 katika mji wa Barcal huko Ubelgiji na alikufa tarehe 09/10/1977 akiwa na umri wa miaka sabini na moja huko huko Ubelgiji. Aliishi Kongo kwa miaka ishirini na tisa mpaka pale aliporejea kwao ubelgiji. Kwa kipindi chote alipokuwa Kongo alifanya kazi kuu mbili, kazi ya umishenari na uandishi.Katika kipindi chote hicho alichokaa Kongo alisoma tabia ya waafrika wanaoishi Kongo hususani kabila la Waruba,...

ZITAMBUE NJIA RAHISI ZA KUTAMBUA JINSIA YA MTOTO ALIYEKO TUMBONI

Image
UTAFITI: ZITAMBUE NJIA RAHISI ZA KUTAMBUA JINSIA YA MTOTO ALIYEKO TUMBONI MWA MAMA MJAMZITO  Mwanamke anapokuwa mjamzito huwa na wasi wasi na kushindwa kugundua kama ujauzito aliobeba ni mtoto wa kike au wa kiume. Kuna njia mbalimbali ambazo wakunga, wataalamu wa afya na wanawaake wazoefu huzitumia kutambua jinsia ya mtoto aliyeko tumboni ambapo mara nyingi asilimia zaidi ya 50 huwa ni kweli. Zifuatazo ni dalili na njia zinazotumika kutambua jinsia:- 1. Tumbo, wazoefu wanaamini endapo utakuwa umebeba uzito mdogo tumboni na tumbo dogo mtoto atakuwa ni wa kume. 2. Haja ndogo, endapo mama mjamzito anatoa haja ndogo rangi nyeusi kuna uwezekano mkubwa amebeba mtoto wa kiume huku nyeupe au rangi ya mawimbi ikimaanisha jinsia ya kike. 3. Chunusi, uwepo wa chunusi nyingi na mara kwa mara ni ishara kuwa umebeba mtoto wa kiume wakati ngozi kuwa laini sana kupita awali ikimaanisha ni mimba ya mtoto wa kike. 4. Maziwa, pale ziwa la kulia linapokuwa kubwa kuliko ziwa la kushoto inamaanisha mimba ...

DIWANI YA ALMASI ZA AFRICA

Image
UHAKIKI WA USHAIRI UCHAMBUZI UTANGULIZI Almasi za Afrika ni diwani iliyoandikwa na Shabani Robert mwaka 1959 katika lugha ya Kiswahili na kuitafsiri katika lugha ya Kingereza kama African Diamonds. Kila shairi limetafsiriwa katika Lugha ya Kingereza kwa lengo la kudhihirisha umahiri wake katika lugha hizi mbili, kuwasaidia wageni wa utamaduni wa Kiswahili kuzifaidi almasi hizi adimu pamoja na kuonesha namna lugha ya Kiswahili isivyo maskini kama baadhi ya watu wanavyodhani na jinsi iwezavyo kuchukuana vyema na lugha nyingine za Kigeni hususani Kingereza. Tafsiri hizo siyo namna ya uandishi wa mashairi ya Kingereza. Hasha! Ushairi wa Kingereza una namna yake ya utunzi tofauti na namna ya utunzi wa ushairi wa Kiswahili. Kwa ufupi diwani hii inazungumzia maadili, utu wema, matendo mema, lugha ya Kiswahili, ujasiri na kujitoa mhanga. Kwa ujumla hizi ndizo Almasi zinazozungumziwa katika diwani hii yenye mkusanyiko wa mashairi kumi na moja ambayo ni Mtukufu Margaret, Wajibu wetu, Sahau,Ra...