Wayahudi katika Historia - Somo la 13 Wayahudi katika Historia - Somo la 13 Submitted by CarlHinton on Sun, 04/06/2014 - 17:23 SOMO LA 13 MASOMO YA WAKRISTADELFIA KWA NJIA YA POSTA   WAYAHUDI KATIKA HISTORIA (Sehemu ya 1)   SOMO: Mwanzo 37   Mwanzo wa historia yao Habari za Wayahudi zinaanza hasa ni yule mtu mmoja aliyekuwa mtu wa imani sana, aliyeitwa Ibrahimu. Alipata mtoto wa kiume wakati wa uzee wake, aliyeitwa Isaka, na Isaka akawa na mwana aliyemwita Yakobo, aliyepewa jina la Israeli baadaye. Yakobo alipata wana kumi na wawili wa kiume, ambao ni mababa wa makabila kumi na mawili ya Israeli.   Mwana wa kiume wa pili kutoka mwisho aliitwa Yusufu, na historia ya maisha yake tunayoipata kwenye Biblia ni ya kusisimua wakati wote tunapoisoma. Lakini ni zaidi ya kuwa historia; inatupa simulizi juu ya matukio muhimu kuhusiana na watu wa Biblia, Wayahudi. Ndani yake tunapata kielelezo cha ajabu cha vile mkono wa Mungu unavyoyaongoza masuala yanayohusu watu wake.   Tunaweza kukumbuka vile kaka zake Yusufu walivyomuuza kuwa mtumwa kutokana na wivu, na vile baada ya kupatwa na majaribu mengi, Yusufu alivyopanda cheo kuwa mtawala wa Misri. Baada ya hapo, kutokana na njaa kali katika nchi ya Kanaani, baba yake na ndugu zake walihamia Misri kulikokuwa na chakula kwa wingi.

Comments

Popular posts from this blog

HIZI HAPA SMS TAMU ZA KUMTAKIA USIKU MWEMA MPENZI WAKO

SMS na MESEJI 900+ za mapenzi

MIAKA 22 SASA TANGU KUZAMA KWA MELI KUBWA YA MV BUKOBA, TANZANI TUMEJIFUNZA NINI?