UUNDAJI WA KAMUSI , MAANA YA LUGHA KIENZO PDF
Dhana ya Lugha kienzo na umuhimu wake katika utengenezaji wa kamusi Katika kujadili mada hii tutaangalia dhana ya lugha kienzo kama ilivyojadiliwa na wataalamu mbalimbali, mifano ya lugha kienzo kutoka katika kamusi, umuhimu wa lugha kienzo na mwisho tutatoa hitimisho juu mada hii. Dhana ya lugha kienzo imejadiliwa na wataalamu mbalimbali, miongoni mwa wataalamu hao ni pamoja na: Bwenge (1995) kama alivyonukuliwa na Mdee (1997) wanasema kuwa lugha kienzo ni lugha au ni mtindo utumikao kufasili au kueleza leksimu za lugha. Kwa kifupi lugha kienzo ni lugha itumikayo kuifafanua au kuifasili lugha. Anaendelea kusema dhima ya lugha za lugha kienzo ni: kueleza lugha kwa ufasaha, utoshelevu , kwa muhtasari na uwazi ili kumwezesha mtumiaji kupata na kuelewa mara moja kile anachokitafuta bila kumchosha akili. Fasili hii inaelezea dhana ya lugha kienzo kwa ujumla katika lugha, lakini hata hivyo kamusi nayo ina lugha inayotumiwa kuelezea taarifa mbalimbali zinazohus...