Posts

DALILI ZA KICHAA CHA MBWA

  Kijue kichaa cha Mbwa KIJUE KICHAA CHA MBWA Na;- SHIRA S.MANGUBE IDARA YA AFYA – KINGA RRH – LIGULA MALENGO YA MADA: Kujua kichaa cha mbwa  Jinsi ugonjwa unavyoenea Muda wa dalili kujitokeza (Incubation period) Kufahamu dalili zake kwa mtu Makundi 3 ya aina ya jeraha Kujua jinsi ya  kuhudumia mtu aliyetafunwa na mbwa mwenye kichaa Kujua  tiba kinga inayopaswa kutolewa kwa mtu aliyeumwa na mbwa anayehisiwa kuwa na kichaa Kujua mbinu zinazotumika kudhibiti ugonjwa wa kichaa cha mbwa  UGOJWA WA KICHAA CHA MBWA NI NINI? Ugonjwa hatari  unaoenea toka kwa wanyama kwenda kwa binadamu (zoonotic disease)   husababishwa na virusi  aina ya RNA kundi la  Lyssavirus , familia ya  Rhabdoviridae.  Kifo ni 100%   kama mtu aliyeumwa na mbwa hatapatiwa tiba kinga JINSI UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA UNAVYOENEA KWA TANZANIA   MBWA NDIYE MWENEZAJI MKUU  WA UGONJWA HUU KWA BINADAMU NA  KWA WANYAMA WENGINE KAMA NG’OMBE NK JINSI UGO...

Mhitimu VETA aanzisha kiwanda chake

Image
  Muhitimu kutoka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dodoma fani ya uchomeleaji, Faraja Michael aanzisha kiwanda chake kutengeneza vitu mbalimbali vinavyotokana na chuma pamoja na Aluminium. Akizungumza katika Banda la VETA kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Michael amesema kuwa katika maisha na elimu yake ya Darasa la Tatu tu hakuwahi kufikiria kuja kuwa na kiwanda lakini kutokana na mradi E4DT ameweza kuanzisha kiwanda cha uchomeleaji. Amesema kuwa ujuzi alioupata sasa anaendesha maisha yake na kuondokana na tatizo la ajira. “VETA imeweza kuniinua kama kijana kupata ajira yangu ya kudumu inayotokana na ujuzi licha ya kuwa darasa la tatu B,” amesema Michael. Amesema kuwa kazi kubwa katika ujuzi ni kujituma na kuangalia kitu cha ziada ambacho jamii inahitaji lakini hawezi kupata.Aidha amesema kuwa vijana wengi wanasema hakuna ajira wakati wakisoma VETA ajira hizo watapata kupitia ujuzi wao....

Utaratibu wa kupima DNA

Image
NA BASHIR YAKUB Hauna haja ya kuvutana na mtu kuhusu iwapo wewe ni baba wa mtoto au hapana. Nimesema baba kwa sababu wasiwasi wa aina hii mara zote upo kwa wanaume. Kuwa fulani ni mama wa fulani karibia mara zote hapana utata. Basi wapo wanaopenda au ambao wangependa kufanya vipimo vya vinasaba (DNA) kuthibitisha kama ni wazazi kweli au hapana. Nitaeleza utaratibu mzima hapa kutokana na Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba vya Binadamu ya 2009, Sura ya 73. 1. Nani anaweza kupimwa DNA? Yeyote ambaye anahitaji kujua kuhusu uhalali wa uzazi wake anaweza kupima DNA. Upimaji huu hauna umri. Hata hivyo DNA si kwa jili ya masuala ya kuthibitisha uzazi tu, bali hutumika hata katika masuala ya ushahidi na upelelezi. 2. Nani ana mamlaka ya kuomba DNA kupimwa? Si kila mtu anaweza kuomba kupima DNA. Hata kama mwenye uhitaji ni wewe lakini bado hauna mamlaka ya kuomba kupima DNA. Kifungu cha 25(2) cha sheria niliyotaja hapo juu kinawataja wafuatao kuwa na mamlaka ya kuomba DNA kupimwa. Kinamtaja hakimu ...

DALILI ZA MWANZO ZA MIMBA NI ZIPI?

 Baada ya kutambuwa siku sahihi ya kutafuta ujauzito sasa ninakwenda kukufahamisha kama mimba iliingia, kama harakati zako zilifahamika. Dalili nitakazokutajia unaweza kuzishuhudiandani ya wiki ya mwanza mpaka wiki ya nne. Hata hivyo kama utakuwa makini unaweza kugundua ndani ya siku chache tu kama sio siku moja ama mbili. Kabla ya kuendelea ningependa utambuwe kuwa mimba huleta mabadiliko makubwa sana kwenye mwili wa mwanamke. Hivyo ni lazima mabadiliko haya yaonyeshe dalili zozote punde tu inapoingia. Hivyo kwa mwanamke akiwa makini na mwii wake anaweza kugundua mabadiliko haya mapema sana. Kuna mwanamke mmoja alinieleza kuwa yeye anaweza kugundua ujauzito kama umetunga ndani ya masaa machache toka akutane kimwili. Nilistaajabu ila nilishindwa kumuuliza anatumia njia gani. Dalili za mimba changa ni pamoja na:- DALILI ZA MIMBA KATIKA WIKI YA KWANZA NA PILI (SIKU 7 MPAKA 14) 1.Kuendelea kwa joto la mwili. Kama ulikuwa makini na siku ambayo j...

JINSI YA KUIMARISHA KINGA YAKO YA MWILI

Image
  UKITAKA kuimarisha kinga ya mwili wako ili kukabiliana na magonjwa ni lazima kufanya mabadiliko katika chakula na mtindo wa maisha ulio nao ili kuimarisha nguvu ya kukabiliana na viumbe hai mwilini ambavyo husababisha maradhi. Vifuatavyo ni vidokezo tisa vya kuimarisha kinga asili ya mwili wako. 1. Pata usingizi wa kutosha Usingizi na kinga ya mwili ni vitu vinavyokwenda pamoja, kwani usingizi usiotosha unahusiana kwa kiwango kikubwa na urahisi wa mtu kupatwa na magonjwa. Utafiti uliofanywa kwa watu 164 wazima ambao hulala  chini ya saa sita kila usiku, umeonyesha kwamba ni rahisi kwao kupata mafua kuliko wanaolala kwa zaidi ya saa sita kila usiku. Usingizi wa kutosha unaimarisha kinga ya mwili, kwani kulala kwa muda mrefu husaidia kinga yako kupambana na ugonjwa ulio nao. Watu wazima wanatakiwa kulala saa saba au zaidi kila usiku ambapo watoto chini ya miaka 20 wanatakiwa kulala saa 8 hadi 10, na watoto wadogo wanatakiwa kulala saa 14. Ukiwa una matatizo...

Maneno ya kumwambia mwanaume wako na kuamsha hisia zake kimapenzi

Image
  Kunong’onezana maneno yalio na mvuto au kuandikiana barua kutuma kwa umpendae, yamepitwa na wakati kwa kizazi hiki, mwanzo vitu hivyo vilikuwa vinaleta mapenzi na hisia za ndani kwa kila mtu. Siku za leo, tuna njia nyingine , bila shaka unaweza kuwa bado unatuma barua na kunong’ona kwa mwanaume kwa maneno matamu kwenye sikio lake. Hata hivyo kwa sasa unaweza kutuma ujumbe kwa kumemail au kwa ujumbe wa kawaida. Hata hivyo , tangu imekuwa na urahisi wa kuwasiliana, kwa nini usijifunze maneno matamu na ujaribu kumtoa katika hali ya huzuni na kumpeleka katika ulimwengu mwingine kwa kuondoa migomo.? Kwa njia hio, kama unapenda kujifunza jinsi ya kuongea hayo maneno na kuugeuza moyo wake, kujenga muungiliano na utulivu na kutunza mawazo yake akiwa kazini akiwa anakuwazia wewe, kwa hio unahitaji kuangalia mbinu zaidi kutoka kwenye makala hii. Lakini kama maongezi matamu ni zaidi ya mtindo wako,- angalia mtiririko huu wa mambo matamu ya kusema kwa boyfriend, kwa vyote kwa upya na mahusia...