Madhara ya kunywa pombe kupita kiasi
UNYWAJI wa pombe kupitia kiasi si mzuri kwa afya yako, kitu kilichothibitishwa kisayansi miaka kadhaa iliopita. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, utafiti umeonyesha kuwa imani za zamani kwamba glasi moja ya mvinyo wakati wa chakula ni muhimu ni potofu. Hivi sasa athari za unywaji wa pombe zinazidi kujulikana. Kundi moja la wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Rutgers nchini Marekani na watafiti kutoka chuo cha Yale nchini humo, wamegundua kwamba unywaji wa pombe unaweza kuathiri chembechembe za vinasaba vya binadamu (DNA) na kumfanya atamani kunywa pombe zaidi. Watu wengi pia wanahoji iwapo kinywaji kimoja kina athari mbaya kwa afya. Ili kupata jibu, kundi hilo la watafiti liliamua kuangazia uchanganuzi wake katika jeni mbili zinazohusiana na kudhibiti tabia wakati tunapokuwa chini ya shinikizo la pombe. Moja ni ile ya PER2 inayoshawishi maisha ya miili yetu na nyingine ya POMC, ambayo inadhibiti utaratibu wetu wa kukabiliana na dhiki. Wakilinganisha wany...