SERIKALI YAGHARAMIA MASHABIKI KUIONA YANGA SOUTH
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu. Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika juhudi za hamasa kuendelea kuunga mkono michezo nchini hususani katika mashindano ya kimataifa, imeamua kugharamia jumla ya mashabiki 55 watakaosafiri kuelekea nchini Afrika Kusini, kwenda kuishangilia klabu ya Yanga katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Marumo Gallants, utakaopigwa Mei 17, 2023 kwenye uwanja wa Royal Bafokeng uliopo katika mji wa Rustenburg nchini humo. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu alipokuwa anazungumza na vyombo vya habari Mei 13, 2023, katika ukumbi wa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa msafara huo wa hamasa utaongozwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Hamis Mwinjuma. “katika hii safari, Serikali imesaidia Yanga kupeleka baadhi ya mashabiki 55 ambao wataondoka leo jumapili ta...