JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME NA WAKIKE

Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX. Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana. Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana Fahamu sifa za chromosomes X na Y za mwanaume. Ili uweze kufanikiwa kuchagua mtoto wa kiume au wa kike lazima ujue sifa za chromosomes hizi zinazoamua jinsia ya mtoto. Sifa za chromosomes Y • Zina spidi kubwa sana kwahiyo kama yai lipo tayari zenyewe zitawahi kwenda kurutubisha • Zina maisha mafupi sana kulinganisha na X Sifa za chromosomes X • Zina spidi ndogo sana • Zina maisha marefu kulinganisha na Y Baada ya kujua sifa za chromosome ambazo ndo zinatusaidia kuamua jinsia twende moja kwa moja kwenye jinsi ya kupata mtoto wa jinsia unayotaka Mambo ya kuzingatia katika suala la kuamua jinsia ya mtoto amtakaye: • Lazima mwanamke ajue mzunguko wake (menstrual cycle)siku ya...