Aibiwa Figo Yake Akiwa Amelazwa Hospitali, Polisi Yatoa Tamko
Muhammad Kabanda, mkazi wa kijiji cha Gangu nje kidogo ya jiji la Kampala NI RAHISI mno kusikia habari za watu kupoteza mali, pesa, marafiki au hata wapenzi wao, lakini ni jambo la kustaajabisha sana kusikia kwamba mtu anaweza akapoteza kiungo cha mwili wake, tena cha ndani katika njia tatanishi. Ndio hali iliyompata mwanaume mmoja kutoka taifa jirani la Uganda ambaye sasa analilia haki baada ya kugundua kwamba figo yake moja haipo tena alipolazwa hospitalini. Kulingana na jarida la Daily Monitor, Muhammad Kabanda, mkazi wa kijiji cha Gangu nje kidogo ya jiji la Kampala anasemekana alitembelea kituo cha hospitali cha Old Kampala mnamo Septemba 24, 2022 kufuatia ajali ya bodaboda kwenye barabara ya Lukuli. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa na majeraha mabaya kichwani ambapo alitakiwa kulipia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji. “Lakini operesheni hiyo ilipofanyika nilishtuka baada ya kugundua kuwa nilichanjwa chale mpya upande wa kusho...