JAMAA ALIYEUA MKE KWA KUMPIGA RISASI MWANZA AJIUA...MKE HAKUPOKEA SIMU ZA MMEWE MARA 37

Swalha enzi za uhai wake Mwanaume aitwaye Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kadhaa mke wake Swalha Salum (28) mkazi wa Kirumba jijini Mwanza usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022 amekutwa amejiua. Wanandoa hao walifunga pingu za maisha Disemba 31, 2021. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Mairi Makori amethibitisha kujiua kwa Said Oswayo ambaye alikuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake umekutwa ndani ya Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza ukiwa na majeraha ya risasi kichwani. Kamanda Makori amesema mwili huo ulikutwa unaelea ufukweni mwa Ziwa Victoria ufukwe wa Rock Beach ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuwatafuta ndugu kwa utambulisho na kuthibitisha kuwa mtu huyo ndiye mtuhumiwa aliyekuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake. Mdogo wa marehemu mwenye umri wa miaka 15 amesema kabla ya tukio hilo lililotokea usiku wa Jumamosi Mei 28, 2022 marehemu dada yake na mume wake (shemeji) Said Oswayo walikuwa na ugomvi huku sauti z...