Posts

Jinsi ya kuepuka kupotezewa muda kwenye mapenzi

Image
Raha  ya uhusiano wa mapenzi ni kumpata mwenza sahihi na kwa wakati muafaka. Unapopishana na muda, unachelewesha maendeleo yako maana mapenzi ni chachu ya maendeleo. Ili uingie kwenye familia, inakupasa uingie katika muda sahihi na mtu sahihi. Kinyume chake utaishia kuchezewa, ukija kushtuka umri unakuwa si rafiki. Utaingia kwenye uhusiano na mtu ili mradi tu na wewe uwe na mtu. Kwa sababu tu unataka na wewe uwe na familia. Lakini kama ungeingia mapema, pengine ungekuwa mbali katika mipango yako. Wengi sana wanajuta kupoteza muda. Wanalia kuingia kwenye uhusiano na mtu ambaye si sahihi. Ukitaka kufanikiwa kwenye uhusiano, hakikisha unampata mtu sahihi na katika muda muafaka. Ukisikiliza simulizi za wanaume wengi kwa sasa, watakuambia wamechoka kuishi maisha ya ubachela. Wanataka kuwa na wenza wao ili kwa namna moja au nyingine, washirikiane katika kutengeneza maisha na wapate maendeleo kabla uzee haujawanyemelea. Wanakiri kwamba kwa kuishia maisha ya ubachela, wanajikuta wakiwa kwe...

MATUMIZI YA NDIZI KATIKA UREMBO

Image
  Mbali na kulika, ndizi zina manufaa mengine, hasa katika urembo wa ngozi. Ndizi zina virutubisho muhimu vinavyoboresha ngozi. Ndizi pia zina aina tatu za sukari zinazojulikana kama ‘sucrose’, ‘fructose’ na ‘glucose’. Hakikisha unanawa uso wako mara tatu kwa siku. Unapofanya hivyo unaondoa uchafu. Ndizi pia husaidia kuzuia chunusi. Hakikisha unanawa uso kwa sabuni ambayo inaendana na ngozi yako. Ikiwa ngozi yako ni ya mafuta, hakikisha unatumia sabuni ambayo itakuacha ukiwa mkavu na kama ngozi yako ina ukavu, jioshe na sabuni itakayokufanya uwe na unyevu. Kulainisha ngozi Changanya asali na ndizi moja iliyopondwa na upake kwenye uso na shingo. Nawa uso kwa maji ya fufutende baada ya muda wa nusu saa. Fanya hivi angalau mara moja kwa wiki. Kung'arisha uso Ndizi huwa na Vitamin C ambayo husaidia kuiweka ngozi kuonekana iking'aa. Kwenye ndizi iliyopondwa, ongeza vijiko viwili vidogo vya juisi ya limau na upake kwa uso na shingo. Osha kwa maji ya fufutende baada ya dakika 20. Ni v...

Mambo ambayo wanawake wengi hudanganya katika mahusiano

Image
  Najua sio raisi kukubali haya, lakini kuna aina ya wanawake ambao ni waongo sana, na hiyo inajulikana, hata kuwashinda wanaume ambao inajulikana wao ndo wajanja katika kudanganya kuliko wanawake, lakini leo tutaangalia vipengele ambavyo wanawake wengi huwa wanadanganya sana kama ifutavyo; Umri Wanawake wengi wanaamini wanaume wanavutiwa na wanawake wenye umri mdogo, wanawake walio na miaka kati ya 24-29 mara nyingi huwa wanashusha miaka 2 hadi 3 ili waonekane wadogo mbele ya wanaume. Kutokuwa na Mahusiano Baadhi wa wanawake, husema wapo kwenye mahusiano hata kama hawapo,hii inatokea hasa kama mwanamke hamtaki mwanaume aliemtokea wakati huo na kisingizio kikubwa ni yeye kuwa katika mahusiano na huu ni uongo mmoja maarufu sana na baadhi ya wanawake pia huwa wanaficha kama wapo kwenye mahusiano, hasa pale wanapotaka kuanzisha mahusiano mapya, huku wakiendelea kuwa na mahusiano na wanaume wawili kwa wakati mmoja. Mara ya mwisho kukutana kimwili na mwanaume Mwanamke hawezi kukwambia u...

THE FUTURE OF AFFILIATE MARKETING ON QUORA, TikTOk AND ODHER SOCIAL MEDIA CHANNELS

  Hello media buyer, affiliate  and martech,  Meet  the golden comment and advice from  proffecianal members  from  top digital ads companies  and agency about  2022 affiliate potentials, they tall about top GEOS, new geos,  top and trending offer for this year, top niches like, mens healithy,  weight loss, and crypto, For me this pdf is very usefull to every  digital marketer  if you want to rise your affiliate income. The pdf is free Get your and read here>> DOWNLOAD ALO PDF 2022 HERE: https://media.alo.events/insights/trends-pdf-2022 ✨ Video about PDF https://www.youtube.com/watch?v=ESujmLR0Mmo&ab_channel=ALO%28AffiliateLeadersOnline%26Offline%29  #ALO #ALO PDF

Madhara ya kukaa, kubana mkojo kwa muda mrefu

Image
    Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature’s call. Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini, akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili. Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo umenibana kweli, ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi ndivyo watu wengi wanafanya. Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia, kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo, mkojo unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa. Kibofu cha mkojo kimezungukw...

UPENDO UNAHITAJI MAMBO HAYA

Image
Upendo unahitaji mambo yafuatayo ambayo ndio msingi wa upendo. Kuna vitu ambavyo upendo unahitaji; 1. Tumaini (Hope) Upendo unahitaji Tumaini, kwa lugha ya Kiyunani ‘elpis’ lenye maana ya (a) Favourable (b) Confident, expectation 2. Uvumilivu (patience) Upendo unahitaji uvumilivu kuvumiliana. Hakuna mwanadamu aliyekamilika katika mambo yote, unajua Waswahili wanasema “mvumilivu hula mbivu “ mvumilivu katika upendo maana yake hii ni shule ya kila siku, tunajifunza kutokana na makosa. Uvumilivu unatakiwa sana katika upendo - unajua kumfanya mwenzi wako kuwa kama wewe unavyotaka awe inahitaji uvumilivu. Hilo ni kweli, maana mmetoka mazingira tofauti na malezi tofauti; hivyo kumbadilisha inahitaji uvumilivu. 3. Kiasi Kiasi ni kitu muhimu. Chochote kinachofinywa zaidi ni hatari, unatakiwa uwe na kiasi katika mambo yako ili uweze kudumu katika upendo maana upendo unahitaji kiasi. Usijifanye uko (busy) sana unakosa hata nafasi/muda wa kukaa na mwenzi wako, lakini wewe unarudi usiku, huo sio u...

KISWAHILI KUTUMIKA KAMA LUGHA YA KAZI UMOJA WA AFRICA

  Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali umeridhia na kupitisha ombi la Tanzania la kutaka Kiswahili kuwa lugha ya kazi katika Umoja huo, Dkt. Mpango amewasilisha ombi hilo la lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kazi katika mikutano ya Umoja wa Afrika. Dkt. Mpango ameongeza kuwa Kiswahili ni miongoni mwa lugha za kiafrika zenye wazungumzaji wengi barani Afrika ambapo takribani watu milioni mia moja wanakitumia Kiswahili pamoja na wazungumzaji kutoka nje ya Bara la Afrika. Kutokana na umuhimu wa lugha hiyo Makamu wa Rais amesema tayari inatumika katika jumuiya mbalimbali ikiwemo jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na kufundishwa kwa lugha hiyo katika nchi nyingi za Afrika Mashuleni. Amesema tayari Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni limetangaza tarehe saba Julai ya kila mwaka kuwa siku ya maadhimisho ya lugha Kiswahili Duniani, Mkutano huo pia umeichagua Tanzania kuwa mjumbe wa Baraza l...