Jinsi ya kuepuka kupotezewa muda kwenye mapenzi

Raha ya uhusiano wa mapenzi ni kumpata mwenza sahihi na kwa wakati muafaka. Unapopishana na muda, unachelewesha maendeleo yako maana mapenzi ni chachu ya maendeleo. Ili uingie kwenye familia, inakupasa uingie katika muda sahihi na mtu sahihi. Kinyume chake utaishia kuchezewa, ukija kushtuka umri unakuwa si rafiki. Utaingia kwenye uhusiano na mtu ili mradi tu na wewe uwe na mtu. Kwa sababu tu unataka na wewe uwe na familia. Lakini kama ungeingia mapema, pengine ungekuwa mbali katika mipango yako. Wengi sana wanajuta kupoteza muda. Wanalia kuingia kwenye uhusiano na mtu ambaye si sahihi. Ukitaka kufanikiwa kwenye uhusiano, hakikisha unampata mtu sahihi na katika muda muafaka. Ukisikiliza simulizi za wanaume wengi kwa sasa, watakuambia wamechoka kuishi maisha ya ubachela. Wanataka kuwa na wenza wao ili kwa namna moja au nyingine, washirikiane katika kutengeneza maisha na wapate maendeleo kabla uzee haujawanyemelea. Wanakiri kwamba kwa kuishia maisha ya ubachela, wanajikuta wakiwa kwe...