Wanne wafariki dunia tukio la kurushiana risasi Dar
Ni baada ya kufyatuliwa risasi na mtu asiyejulikana. Limetokea katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni. Rais Samia atoa pole kwa wafiwa, aagiza uchunguzi kufanyika. Dar es Salaam. Watu wanne wamefariki dunia na sita kujeruhiwa katika tukio la mauaji lililotokea leo mchana katika katika eneo la Selander jijini Dar es Salaam baada ya mtu mmoja kuwashambulia kwa risasi. Katika tukio hilo, lililotokea mchana wa leo Agosti 25, 2021 katika makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni jirani na Ubalozi wa Ufaransa, jijini hapa, mtu huyo asiyefahamika alizua taharuki baada ya kutekeleza mauji hayo huku akifyatua risasi hewani. Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas amewaaambia wanahabari katika eneo la tukio kuwa mtu huyo aliyetekeleza kitendo hicho alidhibitiwa na baadaye kuuawa. “Wakiwa kazini (askari) alikuja mtu mmoja akawashambulia askari hao kwa silaha ya aina ya bastola baada ya kuwashambulia na kuanguka alichukua bunduki zao mbili na kuanza kurusha r...