Posts

Job Opportunities Azam Group at AzamPay - Graduate Management Trainee Program

Image
    Overview AzamPay was founded in 2016 and is a Tanzania-based digital commerce company developing a series of products for the East African market. The company was formed in partnership with the Azam Group of companies and seeks to leverage the Azam brand and presence in East Africa for the purposes of creating value through technology-enabled products and services that can benefit businesses and consumers across the region. The company believes.... A focus on customer service and value in combination with technology that is locally tested and developed can significantly improve the commercial operating environment in East Africa, unlocking tremendous value for local economies. AzamPay is focused on ensuring its approach is rooted in the specific business needs of local communities and is sensitive to expanding access to its services for those who do not have them. East Africa as a region will experience tremendous growth over the next 30 years and AzamPay recognizes an opp...

UHAKIKI WA RIWAYA RIWAYA YA TUTARUDI NA ROHO ZETU?

  1.0   Utangulizi Kazi hii inahusu uchambuzi wa maudhui katika riwaya ya mkondo wa kipelelezi na kiarifu ambayo inaitwa “Tutarudi na Roho Zetu?” iliyoandikwa na Ben Mtobwa. Katika kujadili riwaya hii tutaeleza dhana ya riwaya, dhana ya mkondo wa kipelelezi, usuli wa mwandishi, muhtasari wa kitabuchenyewe, nadharia itakayotumika kuchambua maudhui ya kitabu hiki, uchambuzi wa maudhui na hitimisho. 1.1 Dhana ya Riwaya Kwa mujibu wa Madumulla (2009) akimrejelea Msokile (1992) anafafanua kuwa riwaya ni kazi ya sanaa ya kubuni, ni maandishi ya nathari (ujazo) yanayosimulia hadithi ambayo kwa kawaida ina uzito, upana, urefu wa kutosha, ina wahusika wengi wenye tabia mbalimbali, ina migogoro mingi mikubwa na midogo. Senkoro (1982) anasema riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja, na yenye mazungumzo na maelezo yanayozingatia kwa undani na upana maisha ya jamii. Wamitila (2003), Samwel na wenzake (2013), wanasema kuwa riwaya ni kazi andishi...

UHAKIKI WA FUMO LYONGO KWA KUTUMIA NADHARIA YA VIKALE

  UHAKIKI WA HADITHI YA   FUMO LYONGO KWA KUTUMIA NADHARIA YA VIKALE. Nadharia ya vikale ni mojawapo wa nadharia critical theory.Hii ni nadharia ambayo kuchanganua maandishi hasa visa vya kikale kwa kuelekeza makali yake kwenye ngano za kimiujiza.Mifano ya ngano hizi za kimiujiza ni mighani. Nadharia hii imeelekeza mizizi yake katika miaka ya 1934 wakati Maud Bodkin alipokichapisha kitabu chake, Archetypal Patterns in Poetry. Nadharia hii ina Mihimili yake miwili mikuu katika vitengo viwili vya kiakademia. Vitengo hivi ni Anthropolojia na saikolojia Kila mhimili huchangia nadharia hii katika njia tofauti teule. Saikolojia hujitokeza kama tawi dogo la nadharia hii ya vikale. Nadharia ya vikale ilitia fora mno katika miaka ya 1940 na 1950 kutokana na kazi ya mchanganuzi wa vikale kutoka Kanada, Northrop Frye. Ingawa nadharia hii ya vikale haijatamba na kutaratamba pakubwa, bado inashikilia nafasi kubwa muhimu katika jamii zetu za kiutamaduni. . Usuli wa athropolojia ya...

maudhui ya kazi za kifasihi husawiri jamii halisi

  FASIHI HUCHOTA MAUDHUI YAKE KUTOKA KATIKA HALI HALISI ZA JAMII. JADILI KAULI HII KWA KUREJELEA HADITHI TEULE. Maudhui  katika kazi ya fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii hadi akatunga na kusanii kazi fulani ya kifasihi. Vipengele vya maudhui ni pamoja na dhamira, migogoro, falsafa ujumbe na msimamo.   Mwandishi wa kazi ya fasihi huwa na jukumu kubwa la kuichuja, kuiongoza, kuielekeza au kuikashifu jamii bila kusahau kuisifu mahali pafaavyo. Ikumbukwe kuwa mwandishi yuyu huyu wa kazi ya fasihi huwa kioo cha jamii kiasi kwamba kupitia kwake tunaweza kufahamu hali halisi inayoikumba jamii husika. Hii ni kwa sababu yale yote ambayo mwandishi huyaandika, msingi wake huwa ni jamii ambapo yupo au ameshuhudia swala husika likitendeka. Maudhui haya huwa ni picha halisi ya matukio au matendo katika jamii inayomhusu mwandishi hivyo basi ...