UNAOGOPA KUTOFAUTIANA NA FAMILIA YAKO? TAZAMA FILAMU YA MULAN
Inamhusu binti aliyelazimika kuingia vitani kwa kuigiza kuwa ni mwanamume. Siri yake inapofichuka, analazimika kupigana vilivyo ili arudi uwanjani. Je, atafanikiwa? Atakubalika? Atapona na kurudisha heshima ya familia yake? Dar es Salaam. Ulingoni… Baada ya kikosi chao kuzidiwa na kunasa katika mtego wa adui Bori Khan, ni mpiganaji mmoja tu ndiyo hajanasa katika mtego huo. Ni Hua Mulan ambaye mahesabu yake yanamuonyesha kuwa dakika chache zijazo, wenzake wote watarudishwa nyumbani ndani ya majeneza. Anachokifanya Mulan ni kuokota kofia za wenzake walioaga dunia kwenye mapigano hayo na kuzipanga kwenye mawe. Kisha anaelekeza mshale kwa maadui zake nao wanahisi kuwa wanashambuliwa na kundi la watu waliojificha nyuma yao. Pale wanapoingia katika mtego wa Mulan na kuamua kuhamisha mwelekeo wa mizinga yao, wanajikuta wanapigana na wanajeshi hewa na kuupiga mlima uliojaa barafu na hivyo kusababisha tetemeko linalowasomba wote na kuwafunika na theruji. Subiri kwanza! H...