Dalili za mwanamke asiyekupenda kwa dhati

Unapokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwanamke ambaye hakupendi kwa dhati basi utamgundua kwa dalili zifuatazo; 1. Hataki kuambata na wewe katika matembezi na ikitokea anakuwa mtu wa masharti mara akuambie tangulia nakuja au pengine kutembea nawe kwa umbali. 2. Anapata kigugumizi kukutambulisha kwa rafiki zake na ndugu na inapotokea amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango timilifu. 3. Haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleao, kwake ni kufuja mali na anapokosa kupewa pesa ni mwepesi kulalamika na wakati mwingine kununa kabisa. 4. Anaahilisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi Au kukutungia uongo wa dhahili na kuusisitiza bila kuona aibu. 5. Anapokuwa akitoa maelezo ya mwanaume amtakaye sifa zake zinakuwa hayalingani na wewe. Anaweza kukuambia napenda kuishi na mwanaume mwenye gari au mwenye mwili mkubwa, sifa ambazo wewe huna! 6. Hacheki kwa furaha hata kama ukimchekesha haoneshi furaha ya moyoni. Tena mara nyingine anakuwa m...