Mifumo ya kidijitali itakayokusaidia kufanya kazi nyumbani
Baadhi ya kampuni zinazotoa huduma ya intaneti zimeimarisha huduma hiyo kuwafikia wafanyakazi wanaofanya kazi zao wakiwa nyumbani. Zipo baadhi ya programu tumishi kama Google drive, Meet zinazoweza kuongeza ufanisi wa mawasiliano na kazi. Programu hizo zinasaidia kuwasiliana, kusimamia kazi na kutunza nyaraka mtandaoni. Dar es Salaam. Mlipuko wa ugonjwa virusi vya Corona umeathiri shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii na baadhi ya kampuni na taasisi kulazimika kufunga ofisi na kuwaruhusu wafanyakazi wao kufanyia kazi nyumbani. Hata hivyo, teknolojia ya intaneti na programu tumishi (Apps) zinayafanya maisha kuendelea kama kawaida kwa wafanyakazi kutekeleza majukumu yao popote walipo kwa kuunganishwa na mifumo ya kidijitali. Baadhi ya kampuni za teknolojia ikiwemo ya Liquid Telecom inayotoa huduma ya intaneti nchini Tanzania zimejidhatiti kuhakikisha huduma hiyo inapatikana vizuri ili kazi za uzalishaji ziendelee kama kawaida bila kuathi...