Posts

Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba

Image

Make money online Tanzania

Are you a blogger or site owner and you want to make money online? Use ADSTERA  as alternative of google AdSense. Try to find high C.P.M countries and use direct link or pop under. The adstera pay by minimum of 5$ through pexum, webmoney and PayPal while its pay a minimum of 100$ by local bitcoin. When you want to use wire transfer you must reach 1000$ to your adstera account Click here to Registere JOIN

UN yazidi kukipaisha Kiswahili kimataifa

Image
Yasema ni miongoni mwa lugha inayozidi kupanuka kimatumizi duniani. Dar es Salaam.  Umoja wa  Mataifa (UN) umeipigia chepuo lugha ya Kiswahili kuwa ni miongoni mwa lugha inayozidi kupanuka kimatumizi duniani na kusaidia kueneza utamaduni wake. Katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya lugha mama inayoadhimishwa jana (Februari 21, 2020), Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Audrey Azoulay amesema lugha hiyo imevuka mipaka ya kimataifa na kuwafikia watu wengi ulimwenguni. “ikiwa na wazungumzaji kati ya milioni 120 hadi 150, lugha ya Kiswahili ni moja ya lugha zinazoshamiri kuvuka mipaka ya kule inamozungumzwa. Lugha ya Kiswahili ina maneno kutoka Kusini mwa Afrika, uarabuni, Ulaya na India," amesema Azoulay katika taarifa iliyotolewa na UN. Azoulay amesema ikiwa ni lugha ya Taifa na rasmi kwa Tanzania na pia lugha ya taifa Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Kiswahili pia kinazungumzwa Burundi, ...

VISABABISHI VYA MIMBA KUTUNGWA NJE YA KIZAZI-ECTOPIC PREGNANCY

Image
Kutungwa kwa mimba nnje ya kizazi au kitaalamu ectopic pregnancy hutokea endapo yai lililochavushwa litajipandiki nnje mbali na mfuko wa kizazi. Mimba huanza endapo yai limeshachavushwa,na kwa kawaida hujishikiza kwnye kuta za mfuko wa kizazi baada ya uchavushaji na mbegu ya kiume. Mimba nnje ya kizazi mara nyingi hutokea katika sehemu moja ya njia au mpira wa kubeba mayai kutoka kwenye kiwanda au kwa ovary kwenda kwenye mfuko wa kizazi. Aina hii ya mimba huitwa mimba iliyotungwa katika mrija. Kwa baadhi ya wanawake  mimba hutungwa katika tumbo, kwenye kiwanda cha mayai, shingo ya kizazi  Mimba iliyotungwa nnje ya kizazi  haiwezi kuendelea kama mimba ya kawaida. Yai hili lililochavushwa haliwezi kuishi, na endapo yai likiwa linakuwa huongeza kuharibu mfumo wa kizazi na  endapo itaachwa bila kutibiwa na mama anaweza kupoteza damu nyingi au maisha. Matibabu ya mapema ya mimba il...

Abdul Nondo ajitosa kuwania uongozi ACT-Wazalendo

Image
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, leo Februari 21, 2020 amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa ya ACT Wazalendo. Amesema chama hicho lazima kipate mwenyekiti wa vijana ambaye ataweza kuunganisha nguvu ndani ya chama hicho, kuunganisha vijana kutoka vyama vingine ili kuwa pamoja na kuweza kustahimili mishale itayopigwa na chama tawala.

Ushindani biashara ya chakula mtandaoni wazidi kuibua fursa lukuki Tanzania

Image
Inawarahishia wamiliki wa migawaha na hoteli kuwafikia wateja wao kwa haraka. Inatengeneza fursa za ajira kwa vijana wabunifu wa teknolojia na wasambazaji wa chakula. Wanunuzi nao wanaokoa muda na gharama za kwenda migahawani.  Dar es Salaam.  Baada ya  kampuni ya Jumia iliyokuwa ikitoa huduma za uagizaji wa vyakula mtandaoni kufungasha vilago Tanzania, biashara ya kuuza na kuagiza vyakula mtandaoni imeshika kasi nchini hasa katika jiji la Dar es Salaam, jambo liliongeza ushindani na kufungua fursa mbalimbali za biashara kwa wamiliki wa migahawa na hoteli. Biashara hiyo siyo tu inawafaidisha wasambazaji wa vyakula, bali hata wanunuzi ambao ambao huokoa muda na gharama za kufuata chakula kwenye migahawa badala yake kinawafuata popote walipo kwa kutumia programu tumishi (Apps) kwenye simu zao.  Kadri siku zinavyoenda ushindani unazidi kuchachamaa huku kampuni nyingi za vijana zikiwekeza zaidi katika fursa hiyo mpya ya teknolojia. Baadhi ya programu hiz...

Screen protectors” za simu zaibua mjadala mpana wa ubora Dar

Image
Teknolojia hiyo inajulikana kama “liquid screen protector” hutumika kufunika kioo cha simu kisichubuke au kuharibika haraka. Wafanyabiashara, watumiaji wasema haiwezi kukinga kioo cha simu kisivunjike ikianguka.  Wachambuzi wa teknolojia wasema matumizi sahihi ya teknolojia hiyo yatapunguza changamoto zinazojitokeza sasa.  Dar es Salaam.  Ni saa 4:00 asubuhi wakati jua likiwaka mithiri ya moto wa kifuu, kituo cha daladala cha Makumbusho jijini Dar es Salaam kama kawaida yake kimeshamiri watu na sauti za honi za magari na vipaza sauti vya matangazo ya bidhaa za wafanya biashara wa eneo hilo. Unaweza kuchanganyikiwa! Wakati magari yakiingia na kutoka kituoni hapo, sauti za vipaza za wafanyabiashara zinakuita usogee karibu kwaajili ya kupata bidhaa mbalimbali ikiwemo simu na vifaa vingine vya kielektroniki.   “Ofa ofa ofa, tunabandika “protector za liquid” zinazotumia mitambo ya kisasa, pia tunabandika “protector za 10D na 3D”…,” ni sauti ya kipaza s...