Posts

Uchapaji, uchapishaji wa vitabu Tanzania: kampuni ya uchapaji TRURH PRINTING DAR ES SALAAM

Image
Logo ya truth printing wanaohusika na uchapaji wa vitabu, vipeperushi, mabango, stika, T-shirt, matangazo, bussnes card na nyinginezo Huduma bora za Printing na designing zimekufikia nyumbani/ofisini kwako Vitabu(Books), Vipeperushi, Matangazo, Mabango, Kadi za michango na mialiko, T-shirts, business cards, stickers karibu Truth Printing tukuhudumie ufurahie huduma bora kwa gharama nafuu ndani ya muda muafaka Wasiliana nasi kupitia 0764425704/0652383590 geofreymakula@gmail.com Ubungo DSM. Huduma zinakufikia popote ulipo

Mvua kubwa yaja TMA yatoa tahadhari

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha kwa mvua kubwa katika mikoa mbalimbali nchini  Taarifa ya TMA imesema mvua hizo kubwa zinatarajia kunyesha leo Jumamosi Januari 25, 2020 kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na kusini mwa Mkoa wa Morogoro. “Angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa Mbeya, Njombe, Iringa, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani, Tanga, Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba,” imeeleza taarifa hiyo ya TMA Imesema athari zinazoweza kujitokeza ni uharibifu wa miundombinu na mali kwa baadhi ya maeneo, baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, hatari kwa maisha ya watu kutokana na maji yanayotiririka kwa kasi au maji yenye kina kirefu, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii. Kesho Jumapili Januari 26, 2020 TMA imesema mvua kubwa zitanyesha kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Lindi,...

Umbo, mtindo na muundo wa Riwaya

Muundo wa Riwaya S.A.K. Mlacha Riwaya ya Kiswahili bado ingali changa sana katika upande wa uchambuzi na uhakiki. Historia ya uhakiki wa riwaya ya Kiswahili ambayo imechukua karibu muda wa miaka ishirini hivi sasa, imeonyesha kuwa wataalamu wengi waliofanya uchambuzi wa riwaya ya Kiswahili hawakujaribu kwenda na wakati na kuzitumia njia za kisasa za uchambuzi. Kwa hali hiyo, riwaya ya Kiswahili imebaki nyuma na kuathirika sana kwa upande huo. Wengi wa wahakiki hao wameviangalia vipengele vichache tu kama vipengele huru au mara chache sana wamejaribu kuvihusisha na vipengele vingine kama itakavyojadiliwa hapo baadaye. Mitindo hii ya kuichambua riwaya ambayo ilizoeleka na kuwa ya kawaida kwa karibu kila mwana-fasihi ilionekana kuwa finyu mno. Hii ilikuwa ni kuiangalia riwaya kwa kutumia dhamira, wahusika, lugha au msuko wa matukio bila kujali uhusiano wao kwa pamoja. Kasoro yake kubwa ilikuwa ni kutoikamilisha riwaya kwa vile wahakiki walijikita kwenye kipengele kimoja kimoja t...

Dhana ya Riwaya pendwa: Riwaya pendwa ya kiswahili

Riwaya Pendwa Katika Fasihi ya Kiswahili J.S. Madumulla Katika miaka ya themanini makini ya mhakiki wa fasihi yameelekezwa au kwa usahihi zaidi, yameanza kuelekezwa kwenye aina ya riwaya ambayo hapo nyuma haikupata kushughulikiwa kwa upana kwa sababu ilikuwa haijajitokeza kwa nguvu. Ijapokuwa dalili za aina hii ya riwaya zimekuwako katika fasihi ya Kiswahili tangu miaka ya hamsini, lakini katika miaka ya themanini riwaya hii imejitokeza zaidi. Hata hivyo, kwa kuwa riwaya hii ni 'ngeni' katika Fasihi ya Kiswahili, imekuwa na matatizo kadhaa ya msingi ambayo pindi yakitaaliwa vizuri yanaweza kusaidia kuiainisha na kuibainisha vizuri zaidi. Matatizo hayo ni ya kihistoria, kiistilahi, kifafanuzi, kimawanda, n.k. Kiistilahi Mpaka sasa hapajawa na istilahi muafaka ya Kiswahili ya kuliwakilisha neno la Kiingereza la 'popular literature' au 'popular novel.' Pamekuwa na majina kadhaa kwa ajili ya riwaya hii, kama vile riwaya ya mitaani, riwaya maarufu, riwaya...

Wiki yaisha kwa neema soko la hisa Dar

Image
Thamani ya mauzo yapaa mara 11 ndani ya wiki moja hadi Sh22.6 bilioni wiki iliyoishia Januari 17 kutoka Sh2 bilioni wiki iliyopita. Wachambuzi walieleza awali kuwa sikukuu za mwisho wa mwaka ni moja ya mambo yaliyoathiri wiki mbili za awali za mwaka Dar es Salaam.  Biashara katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imeanza kurudi taratibu katika hali yake baada ya thamani ya mauzo kupaa mara 11 hadi Sh22.64 bilioni katika wiki iliyoishia Januari 17 kutoka Sh2.04 bilioni wiki moja iliyopita. Hali hiyo inakuja baada ya  thamani za mauzo ya wiki mbili  zilizopita kuwa chini kidogo kwa kile wataalamu wa masuala ya hisa na dhamana kueleza kuwa yaliathirika na sikukuu za mwisho wa mwaka. Taarifa ya kampuni ya udalali wa hisa na dhamana Zan Securities imeeleza kuwa kampuni ya bia Tanzania (TBL) ndiyo ilikuwa kichocheo kikubwa cha mafanikio ya soko hilo baada ya kuchangia asilimia 70.65 ya thamani ya mauzo yote kati wiki hiyo iliyoishia Januari 17. TBL imefuati...

BAWASIRI (HAEMORRHOIDS) NI NINI?

Image
Bawasiri ni uvimbe unaoota ndani na/au kuzunguka tundu la kutolea haja kubwa. Awali ya yote, tutaona bawasiri ni nini, kisha tutajadili aina zake, sababu ya uwepo wake na mwisho kabisa, tiba ambazo zinaweza kutolewa kuondoa tatizo hilo. Sehemu ya mwisho ya utumbo mkubwa iitwayo anal canal ina urefu wa kiasi cha sentimeta  4  hivi. Sehemu ya chini kabisa ya anal canal ni tundu la kutolea kinyesi nje ya mwili . Sehemu ya juu yake inaungana na rectum ambayo pia ni sehemu ya utumbo mpana. Kuna mtandao wa veni ndogo (mishipa ya damu) kwenye ngozi inayofunika anal canal. Mara nyingine veni hizi hupanuka na kuruhusu damu nyingi na kuzifanya zitune. Veni hizi zilizotuna na tishu zinazozizunguka zinaweza kutegeneza uvimbe kwenye eneo moja au zaidi, na hii ndiyo huitwa bawasiri, kwa kiingereza  piles   au  pathological hemorrhoids . Kuna Aina Ngapi Za Bawasiri? Bawasiri za ndani  (Internal piles )  ni zile zinazotokea kwenye eneo la ...