Posts

Unayotakiwa kufanya kuepuka madhara ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini

Image
Epuka kukaa au kuegesha vyombo vya usafiri na usafirishaji chini ya miti mikubwa maana matawi au mti vyaweza kuangukia chombo kutokana na ardhi kujaa maji. Watoto, wanafunzi, watu wazima wanashauriwa kutokucheza kwenye kingo za mito kwa kuwa kipindi hiki cha mvua kingo hizo huwa dhaifu hivyo ni rahisi kubomoka au mtu kuteleza na kusombwa na maji. Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka TMA na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na marejeo yake. Dar es Salaam.  Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limewataka wananchi kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo kuepuka kukaa na kuegesha vyombo vya usafiri chini ya miti mikubwa maana wanaweza kuangukiwa na kusababisha madhara.  Machi 29 mwaka huu , Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa katika kipindi cha wiki mbili za Aprili katika maeneo mengi yanayopata mvua za masika hasa mikoa ya mikoa ya...

Nafasi za Kazi 12 TANROADS Tanga

Image
OVERVIEW The Tanzania National Roads Agency (TANROADS) on behalf of the Government of the United Republic of Tanzania entered into a Contract for the Upgrading of Bagamoyo – (Makurunge) – Saadani – Pangani – Tanga (256km) to Bitumen Standard, LOT 1: Pangani – Tanga Section (50Km). The Contract period is 24 months and Defects Liability Period of 12 months.The Regional Manager’s Office TANROADS – Tanga, on behalf of the Chief Executive, TANROADS, intends to recruit qualified and competent Staff to fill the following vacant posts below on specific duties short-term contracts within the Region: Successful applicants must be ready to work for considerable lengths of time in Pangani, Muheza and Tanga Districts within the project area if situations warrant.   POSITION TITLE: MATERIAL ENGINEER (1 POST) Educational/Professional qualifications:- Must be a holder of Bachelor Degree in civil or material engineering from any recognized Higher Learning Instituti...

Haya ndiyo maeneo ambayo watu wanataka kwenda 2019

Image
Kwa mujibu wa Google, maeneo 10 ambayo watu wanapendelea kwenda duniani ni pamoja na kisiwa cha  Maldives  ambacho kimeshika nafasi ya kwanza kutafutwa na watu katika mtandao huo. Picha|  Jennvmy / Unsplash . Kisiwa cha Maldives, Kusini Magharibi mwa nchi za Sri Lanka na India kimeshikwa nafasi ya kwanza kutafutwa zaidi na watu.  Watu wengi wanaotafuta maeneo ya kutembelea, wanapendelea zaidi kwenda Marekani. Dar es Salaam.  Kama tayari au unapanga kutafuta mahali utakapokwenda kutumia mapumziko yako ya mwisho wa mwaka, wewe na umpendaye, basi mtandao wa Google umekurahishia kazi.  Mtandao huo umetoa orodha yake ya mwaka 2019 ya maeneo 10 duniani ambayo watu wengi walikuwa wanatafuta katika kitafutio chake cha “Google Search” kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo mapumziko.  Orodha hiyo ni sehemu ya  watu, mada, matukio, maeneo, na habari za kimataifa ambazo ziligonga vichwa vya watu katika mtandao huo kwa mwaka 2019.  ...

ALIYEACHIWA KWA MSAMAHA WA RAIS AUAWA NA WANANCHI

Image
Mfungwa aliyeachiwa huru kwa msamaha wa Rais kutoka gereza la Bukoba Mkoani Kagera avamia stendi kuu ya mabasi na kuwachoma watu visu ambapo amesababisha kifo cha mfungwa mwenzake aliyeachiwa pia kwa msamaha na majeruhi watano na yeye kuuawa na wananchi wenye hasira kali Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, nakusema tukio hilo lilitokea Desemba 13 mwaka huu majira ya saa tatu usiku eneo la stendi kuu ya mabasi Bukoba Manispaa. Amesema kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa ghafla mtu mmoja asiyefahamika majina yake mwenye umri kati ya miaka (30-35 ) alivamia maeneo ya stendi hiyo na kumchoma kisu tumboni na usoni Godfrey Gobadi ( 35 ) dereva wa bajaji na kumsababishia kifo papo hapo ambaye pia aliachiwa kwa msamaha wa Rais.Malimi amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Michael Bukerebe (26 ) msukuma wa Mwanza fundi magari ambaye amejeruhiwa maeneo ya shingoni na mgongoni, Salum A...

Kwanini unatakiwa kumfuatilia mtoto wako anapokua mtandaoni?

Image
Watoto wanatakiwa kulinda wakati wote wanapoingia mtandaoni. Picha|Mtandao. Ni njia mojawapo ya kumlinda mtoto wa uhalifu wa mtandaoni unaoweza kumpotezea mwelekeo wa maisha. Pia ni kumuepusha na ukatili wa kijinsia unaoweza kukatiza ndoto zake za elimu.  Ni wazi kuwa teknolojia inakua kwa kasi kiasi cha kufanya mifumo ya kujifunza na kufanya mambo kuwavutia watu wengi hasa watoto wenye kudadisi kinachojiri mtandaoni.  Baadhi ya watoto wamekuwa wakitumia simu na kompyuta za wazazi wao kuingia mtandaoni ili kujifunza na kuburudika. Lakini wakati mwingine huwa tofauti kwa sababu baadhi ya mambo yanayopatikana mtandaoni yana madhara kiakili na kiafya kwa mtoto. Hapo ndipo inakuja dhana ya wazazi kuwafuatilia watoto wao wanapokua mtandao ili kujua ni vitu gani wanaangalia na kwa kiasi gani vinachangia kuharibu au kuwakuza katika maadili mema.  Japokuwa bado kuna mjadala katika jamii wa umri sahihi ambao mtoto anatakiwa kuachwa huru bila kuingilia kwa kile...

Filamu za kimataifa zitakazoingia sokoni mwishoni mwa 2019

Image
Miongoni mwa filamu hizo ni pamoja na “Cats” iliyosheheni mastaa wengi wa filamu akiwemo Taylor swift, Jennifer Hudson na Idris Elba.  Filamu za “Jumanji” na “Frozen” nazo zitakuwa sehemu ya kufunga mwaka.  Staa wa filamu Marekani, Will Smith kwa mara nyingine tena atakuwepo katika filamu ya  Gemini Man . Dar es Salaam.  Filamu ni burudani lakini ni sehemu ya kujifunza na kufahamu dunia na tamaduni za watu zinavyoendeshwa. Filamu ni maisha yanayojieleza kwa namna tofauti tofauti.  Wiki iliyopita tulikuletea orodha ya filamu nne ikiwemo ya  Fast and Furious (Hobbs and Shaw)  ambazo zinaendelea kuonyeshwa katika kumbi mbalimbali za Sinema Tanzania. Lakini unahitaji kufahamu mengi zaidi ya filamu hizo.  Leo tunakuletea orodha ya filamu kali ambazo ziko mbioni kutolewa kabla ya mwaka huu wa 2019 kuisha. Kama wewe ni mpenzi wa filamu basi kaa mkao wa kula ili usipitwe na filamu hata moja itakayoingia sokoni. 1.  Jumanji The Next l...

VIDEO | Killy Ft. Alikiba – GUBU

Image