Unayotakiwa kufanya kuepuka madhara ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini
Epuka kukaa au kuegesha vyombo vya usafiri na usafirishaji chini ya miti mikubwa maana matawi au mti vyaweza kuangukia chombo kutokana na ardhi kujaa maji. Watoto, wanafunzi, watu wazima wanashauriwa kutokucheza kwenye kingo za mito kwa kuwa kipindi hiki cha mvua kingo hizo huwa dhaifu hivyo ni rahisi kubomoka au mtu kuteleza na kusombwa na maji. Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri kutoka TMA na kuzingatia tahadhari zilizotolewa na marejeo yake. Dar es Salaam. Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limewataka wananchi kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo kuepuka kukaa na kuegesha vyombo vya usafiri chini ya miti mikubwa maana wanaweza kuangukiwa na kusababisha madhara. Machi 29 mwaka huu , Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa katika kipindi cha wiki mbili za Aprili katika maeneo mengi yanayopata mvua za masika hasa mikoa ya mikoa ya...