Posts

Waziri Mpina Azindua Agenda Za Utafiti Na Kuibua Tafiti Zilizofichwa Makabatini

Image
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua Agenda ya Kitaifa ya Utafiti wa Mifugo, Uvuvi na Ukuzaji wa Viumbe Maji ya mwaka 2020-2025 na kutangaza kuzifumua na kuziibua tafiti zote  zilizofanywa na wasomi na kutelekezwa kwenye makabati miaka ya nyuma na kuziingiza kwenye mfumo rasmi wa matumizi ili kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo. Pia agenda hizo zitaleta msisimko mpya wa kufanya utafiti nchini na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo tafiti nyingi zilifanywa na kutelekezwa kwenye makabati na watafiti mbalimbali wakiwemo Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters Degree)  na Shahada ya Uzamivu (PHD) katika vyuo vikuu mbalimbali. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa agenda hizo kitaifa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),  Kampasi ya Mazimbu mjini Morogoro, Waziri Mpina aliziagiza Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TALIRI) na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi(TAFIRI) kubadilika ili kufan...

Serikali yaamua kumfariji Binti ambae alifichwa kufariki kwa Wazazi Wake Wote na Ndugu Zake Watatu

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, ameeleza kuguswa na tukio la kupoteza wazazi wawili, na ndugu zake watatu lililomkuta mwanafunzi Anna Zambi ambaye amemaliza kidato cha 4 hivi karibuni ambapo Waziri Ummy ameahidi ataenda kumjulia hali mtoto huyo na kumpa salam za pole. Ummy Mwalimu ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake Twitter kufuatia jana mtoto huyo kupelekwa mahali ambapo wazazi wake na ndugu zake wamezikwa baada ya kufariki Dunia walipokuwa wakielekea kwenye Mahafali yake ambapo walifariki Dunia wakiwa mkoani Tanga kutokana na mafuriko ya maji. Waziri Ummy ameandika kuwa; "Suala la mtoto Anna Zambi, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii tunachukua jukumu la kuratibu na kusimamia psychosocial support ya mtoto huyu pamoja na ustawi wake kwa ujumla, Katibu Mkuu Dkt. John Jingu leo ataitembelea familia yake iliyopo Goba” – Waziri Ummy Wazazi walikuwa wakifahamika kwa majina ya Lingston Zambi na Winifrida Lyimo na wadogo za...

FAHAMU ZAIDI KUHUSU KUKABWA NA JINAMIZI (SLEEP PARALYSIS

Image
KUKABWA NA JINAMIZI NINI MAANAA YAKE? Kukabwa na Jinamizi katika ndoto kama tunavyoita ni kitendo ambacho kinawatokea watu wengi sana.  Watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni Jini lakini Tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama “Mwili kupooza katika usingizi” (Sleeping Paralysis) Tendo hilo huwa linakutokea katika muda wa sekunde 20 lakini wewe unayehusika utahisi kama dakika 5 au dakika 10. Matukio hayo ya kijinamizi yanatofautiana na yanakutokea wakati ukiwa nusu usingizini na nusu macho. Ukweli ni kwamba hayana madhara yoyote, ila yanakupa hofu kwa muda fulani. Unapokabwa unakuwa na fahamu nusu. Unaweza kufungua macho, na utahisi kupiga kelele lakini watu hawakusikii, Mwili wako unakuwa hauwezi kufanya lolote na viungo vya mwili wako vinakuwa havifanyi kazi, Inapokutokea unakuwa huwezi kunyanyua mguu wala mkono wala kichwa. Kwa ujumla unakuwa kama uliyepata “ugonjwa wa Kupooza”. Hali hii ya kukabwa inapotokea unaweza ukamuona mtu anayetisha akiingia ndani chumban...

Leviathan kiumbe hatari anayekuja siku ya kiama

Image

Tukio la ajabu watu kuwasiliana na viumbe wa ulimwengu mwengine lilitoke...

Image

Serikali Kumwaga Ajira 16,000 za Walimu

Image
SERIKALI imesema hivi karibuni itatangaza ajira mpya za walimu 16000 wa Sekondari na Shule za msingi ili kupunguza tatizo la walimu katika shule shule hizo, ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu hapa nchini. Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Novemba 14, 2019, Bungeni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya moja kwa moja kutoka kwa wabunge na kuongeza kuwa si upande wa elimu pekee, bali pia wataajiri wauguzi na wahudumu wa afya ili kuboresha huduma hizo kwani serikali imeshafanmikiwa kujenga hospitali na zahanati nchi haopa nchini kipindi kifupi hivyo zinahitaji watumishi. “Serikali imeanza kutoa vibali vya ajira kwenye sekta za Afya, Elimu na Kilimo, na tunakaribia kutoka vibali kwa ajili ya kuajiri walimu 16000 kwa upande wa Elimu za Msingi na Sekondari, vilevile tutatoa vibali vya ajira katika sekta ya afya. “Ununuzi wa korosho msimu 2019/20 utatumia mfumo uleule wa ushirika kwa njia ya minada. Serikali itahakikisha wanunuzi wanalipa vyama vya ushirika kwa w...

Zingatia haya kabla hujanunua bidhaa mtandaoni

Image
Jiridhishe na aina ya kampuni inyotoa huduma ya manunuzi mtandaoni kama ina uhalali. Pitia sera za fidia na kurudisha bidhaa kama zina tija kwako.  Hakiki anuani ya mahali unapoishi ili kuepuka mzigo kupotea. Manunuzi ya bidhaa na huduma mtandaoni yanaongezeka kwa kasi duniani kutokana na ukuaji wa teknolojia na uhitaji wa watu kupata vitu kutoka sehemu tofauti duniani.  Kabla ya kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali mtandaoni, kuna baadhi ya vitu unavyotakiwa kuzingatia ili kupata bidhaa halisi uliyonunua na yenye kukidhi matakwa yako. Izingatiwe kuwa bidhaa za mtandaoni huwezi kuzishika badala yake unaziona kwa picha na taarifa zake. Sasa zingatia haya wakati ukifanya manunuzi yako mtandaoni. Jambo la kwanza kabla hujafanya manunuzi mtandaoni, jiridhishe na tovuti, programu tumishi au mahali unapofanyia manunuzi yako kama ni mfumo unaojulikana na unaweza kukupa bidhaa na huduma unayotaka. Hii itakusaidia kuepuka matapeli ambao wanatumia mtandao kujipati...