UHAKIKI RIWAYA YA TAKADINI PDF
RIWAYA: TAKADINI MWANDISHI: BEN J HANSON WACHAPISHAJI: METHEWS BOOKSTORE AND STATIONERS MWAKA: 2004 MHAKIKI: DAUD MAKOBA MUHTASARI WA RIWAYA Takadini ni riwaya inayojaribu kuzungumzia matatizo ya mila na desturi yaliyopo katika jamii za Kiafrika hasa sehemu za vijijini. Mwandishi anamuonyesha mhusika mkuu Takadini aliyezaliwa na ulemavu wa ngozi jinsi anavyotengwa na watoto, watu wazima na jamii yote kwa ujumla. Mwisho tunamuona Takadini akipendwa na msichana Shingai. Pamoja na vikwazo vingi, penzi la Shingai na Takadini halikufa. Baadae Shingai anapata mimba ya Takadini, kisha anajifungua mtoto asiye mlemavu. Hapo wana jamii wanashangazwa na kujikuta wakiamini kuwa hata mlemavu anaweza kuzaa mtoto asiyemlemavu. UCHAMBUZI WA FANI NA MAUDHUI MAUDHUI KATIKA RIWAYA YA TAKADINI DHAMIRA UKOMBOZI WA KIUTAMADUNI Utamaduni ni jumla ya maisha ya jamii. Katika jamii ya Zimbabwe watu wenye ulemavu hawakuruhusiwa kuishi, waliuawa kikatili. Ni katika jamii hii pia, ...