FASIHI ELETRONIKI MATOKEO YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
MADA: Fasihi Elektroniki: Matokeo ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia Majina ya Mwasilishaji: Wallace Mlaga BA.ED. (UDSM), MA. (UDOM), Mwanafunzi Shahada ya Uzamivu (PhD), OUT Cheo: Mhadhiri , Koleji ya Elimu, Chuo Kikuu cha Rwanda Anwani: P.O.BOX 5039, Kigali Barua pepe: wmlaga@ur.ac.rw Simu ya Kiganjani: +250730584970 1.0. Utangulizi Tungependa kuanza kwa kuuliza maswali yafuatayo: Je, unakubaliana kwamba kugunduliwa kwa maandishi na teknolojia ya uchapishaji kulileta sio tu utanzu mpya wa fasihi andishi bali pia vipera na tanzu mpya za fasihi ambazo hazikuwahi kuwepo hapo kabla? Je, umewahi kujiuliza kwamba maendeleo ya sayansi na teknolojia hususani katika uga wa elektroniki umesababisha kuibuka sio tu kwa utanzu mpya wa fasihi? Uanishaji wa fasihi ya Kiswahili umeshughulikiwa na wataalamu wengi. Miongoni mwao ni pamoja na Mulokozi (1996) na Wamitila (2003). Wataa...