Posts

KUHUSU FURSA ZA KISWAHILI KATIKA NCHI ZA KIGENI, NA DR ANNE JABET KUTOKA CHUO KIKUU CHA VIRGINIA MAREKANI

Image
Dr Anne Jabet Chuo kikuu cha Virginia USA Katika mahojiano mafupi yaliyo fanyika kwa njia ya barua pepe kati ya masheleblog na mkufunzi huyo kutoka chuo kikuu cha Virginia Marekani  amabaye pia ni mjumbe wa CHAUKIDU,  katika mahojiano yaliyo husu fursa mbalimbali katika lugha ya kiswahili katika nchi za kigeni Dk A. Jabet aliithibitishia mashelebog uwepo wa fursa mbalimbali za ajira  na za kimasomo katika nchi za kigeni kwa wasomi wa lugha ya kiswahili Aidha alipo ulizwa kuhusu upatikanaji wa fursa hizo alijibu kuwa fursa hizo hutolewa, Na mhitaji hupaswa kuzitafuta katika mitandao hasa mtambo tafutizi wa Google. Je unaomba fursa za kazi au za kusoma uzamifu? inabidi kuangalia nafasi za kazi mtandaoni kisha kuomba kazi, kunazo kazi mbalimbali hasa za kufunza Kiswahili-umejaribu kuomba nafasi ya fulbright teaching assistant? kama ni nafasi ya kusima inabidi kijaza fomu kupitia idara unayotaka kusomea. natumaini nimejibu swali lako ndug mwandishi. Hayo nd...

AINA ZA BAHARI YA USHAIRI WA KISWAHILI

Image
Na E. MASHELE  +255766605392 BAHARI ZA MASHAIRI Utenzi  Utendi Ndiyo mashairi marefu katika shairi, huwa na kina aghalabu huzungumzia maswala ya kihistoria , mashujaa ,mapenzi na mengineyo. Huwa na kipande kimoja tu. Idadi ya mizani katika kila mshororo huwa kati ya mizani nne na kumi na mbili .kina cha mshororo wa mwisho aghalabu huwa kilele katika beti zote nacho huitwa   kina bahari        Mfano Nakuita hima janabi, Njoo katika ukumbi, Unipeyo rambi rambi, Ya hiki changu kili o , Kilio changu muhubiri, Nataka kukukatibu, Kiwe katika vitabu, Pamo na msaada o , Mifano ya utenzi Utenzi wa fumo liyongo           utenzi wa uhuru wa Kenya  Msuko Ni shairi lenye kibwagizo kifupi. Mfano  i Mwajiona asumini, nanyi mmebahatika, Na waridi vitaruni,mwahisi hamna shaka, Pia viluwanmitini, nanyi mmeburudika, Mtahizika! Mf...

HIZI NDIZO FAIDA ZA VIAMBATA VYA OMEGA 3 NA OMEGA 6 VILIVYOMO KWENYE BLUE BAND MPYA

Image
Wengi wetu tumefanikiwa kuliona Tangazo jipya la Kampuni ya siagi inayofahamika kama BLUE BAND kwenye chanel mbali mbali za TV.Katika Tangazo hilo linaelezea kua BLUE BAND mpya ina Viambata vya OMEGA 3 NA OMEGA 6.Bila shaka watu wengi wamekuwa wakijiuliza Omega 3 ni nini na Omega 6 ni nini,Bila shaka na wewe unayeisoma makala hii ni mmojawapo wa watu wanaojiuliza viambata hivi ni nini. Basi leo nitakuelezea kwa undan nini maana ya viambata hivi na vina umuhimu gani katika afya yako. OMEGA 3 NA OMEGA 6 NI NINI? Omega 3 Hizi ni aina ya Fats(Mafuta) ambazo mwili hauwezi kujitengenezea bali mwili unategemea aina hii ya virutubisho kutoka katika vyakula. Virutubisho hivi vinasaidia utendaji kazi wa Cells zote za mwili,Virutubisho hivi vinasaidia kutengeneza Hormones ambazo zinasaidia kuganda kwa damu pindi unapopata majeraha,Zinasaidia kutanuka na kusinyaa kwa mishipa ya damu hivyo kusaidia kuimarisha mzunguko wa damu. Omega 3 pia inasaidia kuukinga mwili na matatizo ya moyo(heart ...

Wanawake Wanne Wauawa Na Kunyofolewa Nyeti Jijini Mwanza

Image
SIKU moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, kuwaagiza wakuu wa wilaya za Kwimba na Misungwi kupambana na vitendo vya ubakaji na mauaji, wanawake wanne wamekutwa wameuawa kikatili kisha miili yao kunyofolewa nyeti. Miili ya wanawake hao ilipatikana jana ndani ya Shamba la Mifugo la Mabuki, huku ikiwa na dalili za kunyongwa. Mbali ya kupatikana kwa maiti hizo, pia kwenye eneo la tukio kulikutwa mafuvu mawili ya binadamu. Kupatikana kwa maiti hizo kunafanya idadi ya wanawake waliouawa wilayani Misungwi kufikia wanane. Juni 11, mwaka huu, wanawake wengine wanne waliuawa kikatili na watu wasiojulikana ndani ya pori hilo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema miili ya wanawake hao imeshatambuliwa, hivyo akawataka wananchi kutoingia porini kukata kuni wakati Jeshi hilo likiendelea na uchunguzi wa mauaji hayo. Alitoa mwongozo kwamba, katika hatua ya dharura wawepo askari ndani ya shamba hilo kwa ajili ya kufanya doria za kila mara, ikiw...