LEKSIKOGRAFIA NININI?
Katika kulijibu swali hili tutaanza na kutoa fasili mbalimbali kwa mujibu wa wataalamu.Kidahizo kwa mujibu wa TUKI (2001) ni neno linaloingizwa katika kamusi ili lifafanuliwe kwa kupatiwa maelezo yanayohusu taarifa za kisarufi, maana, matumizi, etimolojia, semi mbalimbali za lugha nakadhalika. BAKIZA (2010) Kidahizo ni neno linalochapishwa kwa hati zilizokoza, na pengine kutiwa rangi, kwenye kamusi ambalo taarifa zake zinafafanuliwa. Kutokana na fasili hizi tunaweza kusema kuwa kidahizo ni umbo la msingi linaloingizwa katika kamusi ambamo maumbo mengine yanatokana nalo. Leksikografia kwa mujibu wa Mdee (2010) akimnukuu Wiegand (1984) ni kazi ya kisayansi ya kutunga kamusi. Wikipedia wameifasili leksikografia kuwa ni kazi ya kisayansi na kisanaa ya kutunga kamusi inayojumuisha uorodheshaji wa msamiati wa lugha inayotungiwa kamusi pamoja na maelezo ya kufafanua neon lililoorodheshwa kadri ya watumiaji wa kamusi iliyotungwa. Kutokana na fasili hizi tunaona kuwa leks...