KWANINI WANAUME WENGI WALIOKO KWENYE NDOA HUFA MAPEMA NA KUWAACHA WAKE ZAO???

KWANINI WANAUME WENGI WALIOKO KWENYE NDOA WANAKUFA MAPEMA NA KUWAACHA WAKE ZAO? (Kwanini wajane ni wengi kuliko wagane??) 1. Umri mdogo wa kikomo cha maisha “life expectancy” – Kama unafahamu hili jambo linaloitwa “life expectancy” utakubaliana na mimi kwamba umri wa mwanaume wa kuishi ni mdogo sana ukilinganisha na mke wake, hususani kusini mwa jangwa la sahara. Kwa hiyo wanawake wanapewa nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu kuliko waume zao. 2. Ugumu katika kufunguka – Utakubaliana na mimi kwamba wanaume ni wagumu sana ten asana kufunguka na kushirikisha mambo yao, wao wako tayari wafe na tai shingoni wakijifanya hawaumii au hawasikii shida. Mkiwa na ishu kwenye ndo mkaitwa sehemu muyaongee yeye kamwe hamumpati, anakwambia mambo yetu tutasuluhisha wenyewe wakati ndani yanamla na kummaliza. Na kwa mtaji huu watakufa sana tu 3. Ugumu katika kusamehe – Kusamehe sio tu kwa faida ya anayesamehewa bali pia kwa afya yaw ewe unayesamehe. ...