Posts

Homa ya tumbili yasababisha watu 60 kutengwa

Image
  Watu 60 watengwa kutokana na homa ya tumbili Nigeria Watu 60 wametengwa katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kano, baada ya kukaribiana na watu wanakosiwa kuugua homa ya tumbili au monkeypox. Kamishia wa afya katika jimbo la Kano, Kabul Gesto, alisema kwau moja ya dalili za ugonjwa huo iligunduliwa kwenye mgongwa lakini akasema kuwa ugonjwa huo huenda ukawa homa ya ndege. "Hadi pale matokeo ya sampuni za damu yaliyotumwa kwenda mji mkuu Abuja yatakaporudishwa, hiki kitakuwa kisa cha kushukiwa," alisema wakati wa mahajIano na BBC. Dr Getso anasema kuwa wagonjwa 11 katika majimbo 36 nchini Nigeria wameathirika na homa ya tumbuli. Mamlaka za afya nchini Nigeria zimekuwa zikionya dhdi ya ulaji wa tumbili na nyama ya msituni wiki chache zilizopita. Waziri wa afya Isaac Adewole anasema katika taarifa ya hivi punde kuwa licha ya tiba ya ugonjwa huo kutujulikana hakuma wasi wasi kwa sababu homa hiyo siyo hatari. Hata hivyo amewashauri watu kuchukua tahadha...

MBEYA CITY WATAKA KUMALIZIA HASIRA ZAO KWA SIMBA

Image
TIMU ya Mbeya City imewataarifu Simba SC, kwamba waende Mbeya wakijua wafungwa katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Baada ya sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Simba wanatarajiwa kuwa wageni wa Mbeya City Jumapili Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Na akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo mjini hapa, Meneja wa Mbeya City, Geoffrey Katepa amesema kwamba baada ya kupoteza mchezo wa ugenini dhidi ya Azam FC, hasira zao watamalizia kwa Simba. “Tumefungwa 1-0 na Azam pale Dar es Salaam jambo ambalo ni kinyume na malengo yetu, sisi hatutaki kupoteza mechi, kwa hiyo lazima mchezo wetu unaofuata tushinde ili tujipoze machungu,”amesema. Katepa amesema wanaiheshimu Simba ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri, lakini hata Mbeya City wapo vizuri na kwa kudhihirisha hilo wanataka kushinda Jumapili. “Simba ni timu nzuri, tumewaona hadi Jumamosi walipocheza na Yanga, lakini wanafungika na sisi hapa tutawafunga lazima,”...

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

Image
  CAFFEINA/KAFEINA. Kafeina ni nini?: 1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants drugs’. Utashangaa. Habari ndiyo hiyo. Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina. Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini. Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya. 2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics). Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili. Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisin...

Mganga wa Jadi Mbaroni kwa Kubaka Watoto 14.

Image
  Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia mganga wa kienyeji mkazi wa mtaa wa Minga, Daud Idd (74), kwa tuhuma ya kunajisi watoto 14 wenye umri kati ya miaka saba na 12 na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu zao za siri. Mgonga huyo maarufu kama Babu Karatu ameelezwa kuwa alikuwa akishirikiana kutenda vitendo hivyo na mtoto wa mdogo wake aitwaye Abdallah Yahaya (31). Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumamosi, kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Isaya Mbughi amesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Desemba mwaka jana, hadi Oktoba mwaka huu. Amesema kuwa mwathirika mmoja mwenye umri wa miaka saba siku ya Oktoba 16 mwaka huu saa 11.45 jioni wakati akiogeshwa na mama yake alilalamika kuwa anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri. Amesema baada ya binti kuyo kulalamika kwa mama yake mama huyo aliweza kumchunguza kwenye sehemu zake za siri na kubaini kuwa michubuko inay...

Umeipata Hii? :ZITTO KABWE AMPA NENO NYALANDU BAADA YA KUIHAMA CCM

Image
Nyalandu na Zitto. MBUNGE wa Kigoma  Mjini kwa tiketi ya ACT   Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumpongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Nyalandu  ambaye leo Oktoba 30, 2017 amefanya maamuzi ya kuachana na CCM na kusema kiongozi huyo amefanya maamuzi sahihi.  Zitto Kabwe amesema kuwa kutokana na uchumi unavyoporomoka haki za watu zinavyovunjwa jambo alilofanya Nyalandu ni sawa na kuwa huko ndiyo kuonyesha uongozi.  “Lazaro Nyalandu, umeonyesha Uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na Uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu Sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na Kwa sababu sahihi. Kila la kheri|”  aliandika Zitto Kabwe  Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jam...

Zidane bado ana imani na timu yake

Image
Kocha wa Real Madrid Mfaransa Zinedine Zidane amesema bado timu yake ina muda wa kutosha kuweza kupunguza pointi nane ambazo inazidiwa na vinara Barcelona katika LaLiga msimu huu. Zidane amesema hayo baada ya timu yake kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Girona na kufanya tofauti ya alama kati ya wapinzani hao kuwa nane, Real Madrid ikiwa na alama 20 katika nafasi ya tatu na Barcelona alama 28 kileleni. Licha ya kupoteza mchezo wa pili msimu huu lakini Zinedine Zidane amesisitiza kuwa mabingwa hao watetezi bado wanaweza kutetea ubingwa wao wa La Liga. "Najua tunaweza kurejea kwenye ushindi na tukapata pointi na wengine wakapoteza na tukaongoza ligi kwasababu bado muda ni mwingi na mechi bado ni nyingi mpaka msimu ufike mwisho”, amesema Zidane. Hata hivyo Zidane amegoma kueleza hali ya mlinzi wake Raphael Varane ambaye aliumia kwenye mchezo wa jana ambapo amesema kuwa anasubiri ripoti ya daktari ili kujua endapo atakaa nje ya uwanja au ni maumivu tu ya kawaida na atare...

Zitto Kabwe ataka vyama vya upinzani kuungana

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni kiongozMuu a chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amevitaka vyama vingine vya upinzani ikiwemo CHADEMA, kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanaing'oa CCM kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani. Zitto Kabwe ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni za kuelekea uchaguzi huo, na kusema kwamba wamegundua iwapo wataunganisha nguvu na kuachiana baadhi ya kata, watafanikisha kukitoa chama cha CCM, na hatimaye kutimiza malengo yao ya kushikilia kata hizo. "Iwapo vyama vyote vya upinzani vikituachia sisi kugombea kata za Kijichi tutaishinda CCM, na iwapo sisi tukiwaachia kata ya Mbweni wataishinda CCM, tunaomba wenzetu tuweke nguvu ya pamoja, tushinde Kijichi na Salanga, tumefanya utafiti tumeona tuna nafasi kubwa ya kushinda Kijichi, tuna nafasi kubwa ya kugawa kura na wenzetu Mbweni”, amesema Zitto kabwe Zitto Kabwe ameendelea kusema kwamba ...”Tunawaambia wenzetu kupitia nyie,...