MUSTAKABALI WA MAENDELEO YA KISWAHILI KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Picha/ HISANI P. KIMANI wa Masshele blog Kwa Mukhtasari WAKATI wa kipindi cha kupigania uhuru nchini Tanganyika na kwa kiasi kikubwa Kenya, Kiswahili ndiyo lugha iliyotumiwa kuwaunganisha wakazi wa mataifa hayo. Harakati za siasa zilipoanza kupamba moto nchini Tanganyika, lugha ya Kiswahili ilikuwa 'silaha’ madhubuti iliyotegemewa na chama cha Tanganyika African Association (TAA) kupigania ukombozi. Isitoshe, Chama cha Tanganyika African National Union (TANU) kilipoanzishwa rasmi 1954, viongozi wake walilazimika kutumia Kiswahili mikoani na wilayani kuwashawishi wananchi kujiunga na harakati za ukombozi. Ni sehemu chache sana ambapo lugha za kikabila zilitumiwa na kuhitaji mkalimani wa Kiswahili. Kwa maana hiyo, Kiswahili kilikuwa ni alama ya umoja, uzalendo na uhuru. Hapa Kenya wakati wa utawala wa Uingereza, Kiswahili kilitumika katika baadhi ya shule za msingi hasa ma...