Kuendelea siasa za kupenda vita za Marekani katika Peninsula ya Korea
Katika hali ambayo baadhi ya duru za habari zimearifu kupungua misimamo ya pande mbili kuhusiana na mgogoro wa Peninsula ya Korea, yaani Marekani na Korea Kaskazini, Washington imetuma meli yake ya kivita aina ya USS Ronald Reagan katika maji ya karibu na Korea Kaskazini. Kabla ya hapo pia Marekani ilituma meli ya USS Carl Vinson kwenda katika maji ya Peninsula ya Korea suala ambalo lilisababisha kuongezeka mvutano katika eneo hilo. Korea Kaskazini iliitaja hatua ya kutumwa meli hiyo katika maji ya eneo hilo kuwa ni sawa na kutangaza vita huku ikiionya vikali Washington kutokana na madhara makubwa yanayoweza kutokea kufuatia hatua hiyo ya kichokozi. Mbali na Pyongyang, Uchina pia ilikutaja kupenda vita kwa Washington katika eneo hilo kuwa kunatokana na siasa za kiuhasama za baharini ambapo ilimtaka Rais Donald Trump wa Marekani kuachana na mwenendo huo. Kiongozi wa Korea Kaskazini akikagua marubani wa kike Kwa kuzingatia indhari za mara kwa mara za Korea Kaskazin...