UHAKIKI WA NADHARIA YA KI-MARKS KATIKA FASIHI
UHAKIKI WA NADHARIA YA KI-MARX KATIKA FASIHI. Swali. Eleza mawazo makuu yanayojitokeza katika nadharia ya Umarx kisha hakiki Tamthilia ya Kwenye Ukingo wa Thim kwa kutumia nadharia ya Ki-Marx. DONDOO: UTANGULIZI Maana ya Nadhari Maana ya Umarx Maana ya Nadharia ya Umarx KIINI Mawazo makuu yanayojitokeza katika nadharia ya Umarx. Sifa na udhaifu wa nadharia ya Ki-Marx Uhakiki wa Tamthilia ya Kwenye Ukingo wa Thim. · HITIMISHO · MAREJEO Nadharia ni dhana iliyofafanuliwa na wataalam mbalimbali kama ifuatavyo: Wafula na Njogu,(2007:7) Nadharia ni jumla ya maelekezo yanayomsaidia msomaji au mhakiki kuifahamu kazi ya fasihi kwa kufuata utaratibu maalumu. Tuki, (2004:300) Nadharia ni mawazo, maelezo au muongozo uliopangwa ili kusaidia kueleza, kutatua au kutekeleza jambo fulani. Tunakubaliana na fasili iliyotolewa na Wafula na Njogu, kutokana na kwamba fasili hii imetaja vitu muhimu kama vile, maelekezo ambayo ndiyo yanayomuongoza msomaji au mhakiki ili asivuke mipak...