MAPYA KUTOKA WIZARA YA ELIMU
 Mabadiliko Elimu ya Msingi Yaja, Yaweza kuwa mwisho wa darasa la sita, masomo yapunguzwa 10:55 AM ELIMU No comments   SERIKALI imefanya mabadiliko makubwa katika mitaala na mfumo wa elimu ya msingi, MTANZANIA imebaini. Habari za uhakika kutoka vyanzo vya kuaminika na kuthibitishwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, zinasema mabadiliko hayo ambayo utekelezaji wake unaanza leo, yatagusa aina ya masomo yatakayofundishwa kuanzia darasa la tatu. Kwa mujibu wa habari hizo, upo uwezekano wa elimu ya msingi ambayo imekuwa ikitolewa kwa miaka saba, ikapunguzwa na kuwa miaka sita kwa wanafunzi walioko darasa la tatu hivi sasa. Habari hizo, zinasema masomo yatakayofundishwa kuanzia leo ni Kiswahili, Hisabati, English, Maarifa ya Jamii, Uraia na Maadili, Sayansi na Teknolojia na somo la dini. Lakini pia kutokana na mabadiliko hayo, Serikali imeongezea masomo mawili ya ziada kwa wanafunzi wa darasa hilo ambayo ni Elimu ya Sanaa na Michezo na Vilabu vya Masomo ya Usajariama...