Posts

Early Settelement in AMERICA

Image
     contact us | site guide | search                            SETTLEMENT Resource Menu    Topic Framing Questions • What motivated the Europeans in their initial settlements? • How did the European nations differ in their vision of a successful settlement? • How did they differ in the institutions they created to maintain their settlements? • What factors led to the survival or abandonment of a settlement? • What relationships evolved among European settlers, Native Americans, and enslaved Africans? • What did "America" signify to Europe in 1630? What did "Europe" signify to Native Americans and enslaved Africans?   1. First Arrivals» Reading Guide - Spanish: Columbus's first settlement in the New World, 1493 - English: The first months of the Jamestown colony, 1607 - English: The first year of the Plymouth colony, 1620-21 - Artifacts: Isabella Jamestown Plymouth When we talk about the European s...

UMEWASIKIA AZAMU !

Image
Huku timu za Yanga na Simba zikianza kambi zake leo Jumatatu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, wapinzani wao Azam FC bado wapo majumbani wakisubiri kurejea kwa kocha wao Mhispania, Zeben Hernandez, Desemba 5, mwaka huu. Zeben kwa sasa yupo kwao Hispania alipokwenda mapumziko kabla ya kurejea nchini kuendelea na kibarua chake cha kuiongoza timu hiyo kwenye mzunguko wa pili ambao umepangwa kuanza Desemba 17. Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd, alisema licha ya wenzao hao kuanza kambi mapema, kwa upande wao wanamsubiria kocha wao Zeben arejee kutoka kwao Hispania, ndipo waanze kambi yao. “Kocha wetu atatua nchini Desemba 2 na kambi rasmi tunatarajia kuanza siku tatu mbele yaani Desemba 5, ambapo tunaamini tukirejea tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri, kwa sababu kikosi kimeimarika tofauti na mara ya kwanza ilivyokuwa. “Akishatua hapa nchini ndipo mambo mengine yataendelea ukiwemo usajili wa wachezaji ambao tunawataka kabla ya kufungwa dirisha hili, ambao tuliu...

Nina deni la ubingwa simba :AMESEMA BAADA YA KUMALIZANA NA SIMBA

Image
» BAADA YA KUMALIZANA NA SIMBA, ZIMBWE AWEKA WAZI KWAMBA DENI LIKO KWAKE, ANATAKA UBINGWA SIMBA BAADA YA KUMALIZANA NA SIMBA, ZIMBWE AWEKA WAZI KWAMBA DENI LIKO KWAKE, ANATAKA UBINGWA SIMBA  ZIMBWE JR AKIWA NA RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA MARA BAADA YA ZOEZI LA MKATABA KUKAMILIKA. Baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili, beki wa pembeni wa Simba, Mohamed Zimbwe maarufu kama 'Tshabalala', ametamka kuwa haidai timu hiyo lakini yenyewe ndiyo inamdai deni kubwa la kuhakikisha anaipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu. Tshabalala alisaini mkataba huo wiki iliyopita baada ya ule wa kwanza kubakiza miezi sita. Beki huyo anayecheza namba tatu, kabla ya kusaini mkataba huo alikuwa akiwaniwa vikali na Yanga ambayo ilitenga kitita cha Sh mil 60 ili kumnasa. Hata hivyo, Simba inafanya siri kuhusu dau ililompa ili amwage wino. Tshabalala alisema amepanga kuitumikia timu hiyo kwa mafanikio makubwa katika kipindi chote atakachokuwepo Simba. Tshabalala alisema, moja ya mafanikio atakayoanza...

SAMATTA APATA PIGO ULAYA

Image
KRC GENK YA SAMATTA YAPIGWA BAO 6-0 LIGI KUU YA UBELGIJI KRC GENK YA SAMATTA YAPIGWA BAO 6-0 LIGI KUU YA UBELGIJI  Unaweza kusema siku ya kufanya nyani, miti yote huteleza na ndicho kilichowatokea KRC Genk anayochezea Mtanzania, Mbwana Samatta. Samatta ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea TP Mazembe wakiwa mabingwa wa Afrika, alicheza kwa dakika 90. Genk imepoteza mchezo wake wa Ligi Kuu ya Ubelgiji kwa kuchapwa mabao 6-0 dhidi ya Oostende. Mechi hiyo ilionekana ya upande mmoja na hasa kipindi cha pili ambacho wenyeji walipata mabao yao manne baada ya kungoza 2-0

MAANA YA FONETIKI

Image
FONETIKI AU UTAMKWAJI WA SAUTI-FONIMU ZA KISWAHILI SANIFU FONETIKI AU UTAMKWAJI WA SAUTI-FONIMU ZA KISWAHILI SANIFU MWIZA PETER - 02:36  3.2.1 Maana Ya Fonetiki Fonetiki ni taaluma inayojishughulisha na jinsi sauti yo yote inavyotolewa au inavyopatikana. Hii ni sayansi huru ambayo inatumia nadharia za sayansi halisi kama vile fizikia, uhandisi, baiolojia, nk. na kufaidi matokeo ya kiutafiti ya taaluma hizi. Mathalani, ili mwanafonetiki aelewe jinsi ala za sauti zinavyofanya kazi wakati wa utolewaji wa sauti, atafaidika na maelezo ya kibaiolojia kuhusu namna mfumo wa mwili wa mwanadamu unavyofanya kazi. Mgulu, (2001:48) anadai: ‘ ... fonetiki ni moja tu, lakini fonolojia zipo nyingi kama lugha zenyewe zilivyo nyingi. Kwa mfano, hatuna fonetiki ya Kiingereza au fonetiki ya Kiswhili. Fonetiki ni fonetiki tu. Kwa upande mwingine, tuna fonolojia za lugha mbalimbali ambazo hutofautiana. Tunazo, kwa mfano, fonolojia ya Kiswahili, fonolojia ya Kiingereza, fonolojia ya Kifaransa, ...

ALOFONI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

ALOFONI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI ALOFONI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI) 1.0 UTANGULIZI Alofoni katika lugha ya Kiswahili ni dhana ambayo haijashughulikiwa vizuri. Hii ni kutokana na wataalamu mbalimbali kutofautiana juu ya dhana hii. Tofauti hizi za wataalam zinajitokeza juu sauti za lugha wanazozitoa kama mifano ya alofoni za Kiswahili. Wengine huenda mbali na kusema kuwa lugha ya Kiswahili haina Alofoni. Madhumuni ya makala hii ni kujaribu kuchunguza alofoni katika lugha ya Kiswahili. Na kufikia hitimisho iwapo lugha ya Kiswahili ina Alofoni au la. Na iwapo lugha ya Kiswahili ina alofoni basi alofoni hizo ni zipi? Tutachunguza dhana ya alofoni kama inavyofasiliwa na wataalam mbalimbali, mbinu mbalimbali za kuzitambua alofoni na fonimu za lugha na kisha tutaichunguza mifano mbalimbali ya alofoni inayotolewa na wataalam mbalimbali. Mwisho nitatoa msimamo wangu na kuhitimisha kwa kuchokoza mjadala. 2.0 KIINI Kabla ya kusema Alofoni ni nini kwanza tutoe maana za istilahi za muhimu katika ku...

ISIMU FONIMU INAVYOWEZA KUVUKA MPAKA WA FONIMU NA KUINGIA KATIKA FONIMU NYINGINE

ISIMU FONIMU INAVYOWEZA KUVUKA MPAKA WA FONIMU NA KUINGIA KATIKA FONIMU NYINGINE. Dhana ya fonimu ni dhana ambayo imejadiliwa na wataalamu mbalimbali wakitumia mitazamo tofauti tofauti. Wataalamu wafuatao wameeleza maana ya fonimu:- Massamba, (2004) anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho kina sifa pambanuzi kuweza kukitofautisha na vipande vingine vya aina yake. Sauti pambanuzi katika mfumo wa lugha. Massamba na wenzake, (2004) wanasema fonimu ni kitamkwa kilicho bainifu katika lugha fulani maalumu. Mgullu, akimnukuu Jones, (1975) anaeleza kuwa Fonimu ni kundi la sauti katika lugha fulani, lenye sauti muhimu (phonemes) pamoja na sauti zinazohusiana na ambazo hutumiwa mahali peke katika muktadha maalumu. Tunaweza kusema kuwa wataalamu hawa wametofautiana katika kuelezea dhana nzima ya fonimu, wakati Massamba (2004), anasema fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha, Jones (1975) akinukuliwa na Mgullu anasema kuwa fonimu ni kun...