Posts

KAZI YA INI (funtion of liver)

Image
KAZI YA INI MWILINI INI: Ini ni kiungo muhimu sana katika mwili wa mwanadamu. Ni kiungo ambacho kinahitaji kulindwa na kukingwa pamoja na kusafishwa mara kwa mara. KAZI YA INI MWILINI 1. Ini lina kazi ya uchujaji wa sumu, inachuja sumu kwenye damu ambayo huingia kwa njia ya vyakula, vinywaji (bila kusahau vinywaji vikali), hewa tunayovuta, sigara, pamoja na dawa tunazotumia. 2. Vile vile, hutoa nyongo ambayo kazi yake kubwa ni kusaga mafuta na protini kutoka kwenye chakula tulacho. 3. Pia, ini hukibadilisha chakula na kufanya tupate nguvu mwilini. Hivyo basi, tunahitaji kulilinda ini ili liweze kufanya kazi yake ya uondaji wa sumu na kusaga mafuta na protini kama ilivyokusudiwa. Mara nyingi imeonekana kwa mtu mwenye shida ya ini kuwa akijisikia uchovu mara kwa mara hata kama hajafanya kazi za kuchosha. Hii tutokea kwa kuwa ini limezidiwa na haliwezi kufanya kazi yake ya kuhakikisha mwili unapata nguvu. VYAKULA VINAVYOLINDA NA KUSAFISHA INI 1. Kitunguu saumu: Inasaidia ini kutoa...

Ugonjwa wa ngiri

 Ngiri au 'Hernia' ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi  na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo. Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni). Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa sababu ambazo huweza kumfanya mtu apate ugonjwa wa ngiri ni pamoja nak Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua. Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika Wengi wa waathirika wa tatizo hilo hufanyiwa upa...

UJUE UGONGWA WA BUSHA

Image
SOMA HAPA UJUE CHANZO NA MATIBABU YA UGONJWA WA BUSHA.                                                                                                                                 busha ni nini?                              huu ni uvimbe kwenye korodani ambao unasababishwa na kujaa kwa maji kwenye moja ya sehemu zinazounda korodani kitaalamu kama tunica vaginalis..busha hutokea pale maji yanayotengenezwa kwenye korodani kua mengi sana kuliko yale yanayo ondolewa. busha huweza kutokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa lakini mara nyingi hupotea baada ya muda mfupi tu, kama ukiona halipotei  kwa mtoto wako ni vizuri kuonana na daktari. chanzo cha busha ni nini? kuna aina kuu nne za vyanzo vya busha kama ifuatavyo. idiopathic; hii ni busha inayotokea tu bila hata kujua chanzo ni nini. kuumia; busha huweza kutokea sababu ya kuumia kwa kupigwa na kitu kwenye korodani au kuanguka na kuumiza sehemu hizo. uvimbe; uvimbe kama wa kansa huweza kusababisha busha. magonjwa; ugonjwa unao am...

DK MANDAI: KAMA UNASHIDA YA MIGUU KUWAKA MOTO BASI HII INAKUH...

DK MANDAI: KAMA UNASHIDA YA MIGUU KUWAKA MOTO BASI HII INAKUH... : Matatizo ya aina hii mara nyingi huwapata watu ambao shughuli zao huwalazimisha kutembea kwa muda mrefu, kusimama kwa muda mrefu a...piga simu 0766605392

UVIMBE TUMBONI

Image
MATIBABU YA MAGONJWA MBALIMBALI YALIYOSHINDKANA Sunday, October 11, 2009 UVIMBE WA TUMBONI Uvimbe ni kitu kidogo sana katika tumbo tunaweza kuusawanisha na mchanga lakini huu uvimbe ni mkubwa sana ungiapo kwa motto wa kike na unaweza hata kumuuwa asipokuwa makinini sawa uonavyo na mchanga ukuingipo katika jicho ni kiasi gain unavyowasha tena waweza kufikili umewekewa tofali ndani ya jicho lakini kakitolewa ni kamchanga kadogo sana,sasa hiyo hali ndio imtokeavyo motto wa kike nah ii hali ni mbaya sana kwani huu uvimbe waweza kumsababishia hata kutopata motto kwa sababu huu uvimbe hukaa sana chini ya kizazi mara nyingi sana hupendelea kukaa sehemu kama hizo ukiukosa sehemu ya uzazi hukaa katka mirija ya uzazi sehemu hizi mara nyingi sana hupendelea kwa hivyo sehemu kama hizo kati hizo uvimbe ukaa mara nyingi sana husumbuka sana motto wa kike bora uvimbe huo ukae tofati na hapo lakini iwapo ukakaa eneo zingine maumivu yake huwa ni madogo sana na unaweza usigigungue kama unauvumbe . DALIL...

UGONJWA WA FIBROIDS (uvimbe kwenye kizazi)

Image
Fibroids ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha unaoota na kukua kwenye uterus. Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Fibroids ni uvimbe ambao mara nyingi (asilimia 99) hauna madhara kiafya na wala kuhusiana na ugonjwa wa kansa. Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 30 hadi 50, wana fibroids ingawa wengi wao hawahangaiki kuchukua vipimo vya fibroids. Uvimbe wa fibroids unakuwa na ukubwa tofauti tofauti, unaweza kuwa mdogo kama harage au kufikia ukubwa wa tikiti maji.   Chanzo Cha Fibroids   Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen....

MAGONJWA YA MOYO

Zifahamu aina za Magonjwa ya Moyo, Dalili zake na Njia za Kujikinga Posted By Dr. Joachim Mabula - May, 5th 2015 (6900) Views MAGONJWA ya Moyo (Cardiovascular Diseases), ni miongoni mwa magonjwa yaliyoko kwenye kundi la ugonjwa usioambukiza. Haya ni magonjwa yale yote yanayoathiri moyo na mishipa yake. Kwa hiyo, magonjwa ya moyo yanajumuisha ugonjwa wa Kupanda kwa Shinikizo la Damu (High Blood Pressure/Hypertension). Hili ni tatizo sugu la kiafya linalohusisha kuongezeka kwa mgandamizo wa msukumo wa damu kwenye mishipa ya damu. Magonjwa mengine ni Koronari za Moyo (Coronary Heart Diseases). Huu ni ugonjwa wa moyo ambapo mafuta yanaganda ndani ya ateri koronari na kuziba kwa kiasi fulani au kuziba kabisa kwa ateri ya koronari ya/za moyo, hivyo kusababisha upungufu wa damu katika sehemu ya moyo ambayo hupata damu kupitia mishipa hiyo. Ugonjwa huu wa Koronari za Moyo hudhoofisha misuli ya moyo kiasi cha kusababisha moyo kushindwa kusukuma kiwango cha kutosha cha damu (Heart Failure)....