Posts

Showing posts from February, 2025

Zaidi ya Methali 600 za kiswahili

Image
  Methali ni semi zenye mafunzo fulani , mara nyingi hutumika kuonya na kuipa jamii mwelekeo. Methali huweza kutofautiana kutoka jamii moja na nyingine zenye utamaduni tofauti. Methali pia huweza kubeba tajiriba fulani ya mazingira. METHALI MIA SITA NA KUMI (610) Aanguaye huanguliwa. Asiye sikia la mkuu, huvunjika guu. Abebwaye hujikaza. Adhabu ya kaburi aijuae maiti. Adui aangukapo, mnyanyue. Adui mpende. Adui wa mtu ni mtu. Afadhali ya Musa kuliko ya Firauna. Ahadi ni deni. Ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke. Akiba haiozi. Akili ni mali. Akili ni nywele kila mtu ana zake. Akili nyingi huondowa maarifa. Akutukanae hakuchagulii tusi. Akipenda chongo huita kengeza. Akufaae kwa dhiki, ndiye rafiki. Akufanyiaye ubaya, mlipe wema. Akupaye kisogo si mwenzio. Akutendaye mtende, mche asiyekutenda. Alisifuye jua, limeuangaza. Aliye juu msubiri chini. Aliye kando, haangukiwi na mti. Aliye kupa wewe kiti (kibao) ndiye aliye nipa mimi kumbi. Aliye kutwika, ndiye atakaye kutua. Akufukuz...