SIFA ZA KONSONANTI, UZIADA KANUNI ZA KIUSILIMISHO NA ZISIZO ZA KIUSILIMISHO
SIFA KUU ZA KONSONANTI Sifa hizi zinazingatia mambo makuu matatu 1. Jinsi konsonanti zinzvyotamkwa 2. Mahali ambapo konsonanti hutamkiwa 3. Hali ya nyuzi sauti SIFA ZA JINSI YA MATAMSHI Katika sifa hii konsonanti hugawika katika makundi sita A. VIPASUO/VIZUIWA Wakati wa utamkaji wa konsonanti hizi huwa kuna mzuio wa mkondohewa na kuachiwa ghafula. Konsonanti hizi zimepewa jina hilo kutokana na kwamba katioka kuachiwa ghafla kwa mkondohewa sauti itokeayo huwa kidogo kama ina mlio wa kupasua. Kwa mfano konsonanti /p/, /b/, /t/, /d/, /k/ na /g/. /p/ kipasuo sighuna cha midomo /b/ kipasuo ghuna cha midomo /t/ kipasuo sighuna cha ufizi /d/ kipasuo ghuna chaa ufizi /k/ kipasuo sighuna cha kaakaa laini /g/ kipasuo ghuna cha kaakaa laini B. VIZUIO/VIPASUO KWAMIZA Konsonanti hizi zinapotamkwa hewa husukumwa nje kwa nguvu na kuzuiwa halafu nafasi ndogo huachwa ili hewa ipite ikiwa na mkwa...