Chimbuko la lugha ya kiswahili
Chimbuko ni istilahi yenye maana ya kitu fulani kilipoanzia. Ni dhahiri kuwa kuna mijadala ya wataalamu mbalimbali inayozungumzia chimbuko la lugha ya Kiswahili. Baadhi ya wataalamu hao ni pamoja na Chami (1994), Massamba na wenzake ( 1992 mpaka 1996), Freeman Granville (1959) na wengineo. Ifuatayo ni mitazamo yao kukusu chimbuko la lugha ya Kiswahili. Chami (1994), Massamba na wenzake (1992 hadi (1996) wanasema utafiti uliofanywa na wataalamu wanaosema kuwa chimbuko la lugha ya Kiswahili ni Kingozi kizungumzwacho Kenya na Kishomvu kizungumzwacho maeneo ya Bagamoyo na Dar es Salaam hauna mashiko, hivyo basi litakuwa ni jambo la busara kama watafanyia upya utafiti wao. Nae Freeman Granville (1959) Katika kitabu chake alichokiita "The Medieval of Kiswahili Language" anasema Kilwa hata kabla ya karne ya 10 ilikuwa na umuhimu mkubwa kibiashara, hivyo basi kulingana na umuhimu huo wa kibiashara miongoni mwa Wabantu wa Kilwa na wageni (Waarabu) ilipelekea kuibuka kwa lugha m...